Kwa mujibu wa orodha ya
FIFA ya ubora wa soka duniani iliyotolewa leo nchini Uswizi, zile timu zilizopo
3 Bora, Spain, Germnay na Argentina bado zimeshikilia nafasi zao.
Tanzania inayoongozwa na
taifa stars chini ya kocha mkuu Kim Paulsen imepanda juu nafasi tatu na kujikita
Nafasi ya 116.
Katika miezi miwili,
Tanzania imepanda kwa kasi kutoka nafasi ya 127 mwezi machi na kwenda nafasi ya
119 mwezi Aprili na sasa imekalia nafasi ya 116 baada ya kushusha kipondo kwa
Simba wasiofugika kutoka pwani ya magharibi mwa Afrika, timu ya taifa ya
Cameroon bao 1-0 uwanja wa taifa, na baadaye kuwatungua simba wa milima ya
Atlas, timu ya taifa ya Morroco mabao 3-1 katika mchezo wa kuwania kufuzu
fainali za kombe la dunia.
Wakati Tanzania ikipanda
nafasi tatu juu, Simba watatu yaani timu ya taifa ya England imeporomoka nafasi
3 na sasa ipo nafasi ya 7 huku wazee wa Samba na waandaaji wa michuano ya kombe
la dunia mwakani, timu ya taifa ya Brazil ikiporomoka nafasi 1 na sasa ipo ya
19.
Timu toka Barani Afrika
ambayo iko juu sana ni Tembo wa pwani ya magharibi ya Afrika, timu ya taifa ya
Ivory Coast iliyopanda nafasi 1 na sasa ipo nafasi ya 12.
Orodha nyingine ya timu
bora za taifa duniani itatolewa na FIFA Mei 9 mwaka huu.
BOFYA HAPA
20 BORA:
1 Spain
2 Germany
3 Argentina
4 Croatia
5 Portugal
6 Colombia
7 England
8 Italy
9
Netherlands
10 Ecuador
11 Russia
12 Côte
d’Ivoire
13 Greece
14 Mexico
15
Switzerland
16 Belgium
17 Uruguay
18 France
19 Brazil
20
Denmark
EmoticonEmoticon