MWALIMU JIJINI MBEYA ATUHUMIWA KWA KUMWAMBUKIZA MWANAFUNZI VVU....

 
 IMEELEZWA kuwa mwanafunzi wa Kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Vanessa (jina linahifadhiwa) iliyopo Mkoani Mbeya aliyekuwa na mahusiano ya kingonona  mwalimu wake aitwaye   John Mapunda ameambukizwa virusi vya UKIMWI (VVU).

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka (17) wakati anahusiana kingono na mwalimu wake alikuwa anajiandaa kufanya mtihani wa Taifa wa kidato cha pili mwaka 2012 lakini hakuweza kufanya mtihani huo.

Uchunguzi unaonesha kuwa, Mwalimu Mapunda alikuwa na uhusiano wa kingono na mwanafunzi wake tangu mwaka 2011 akiwa kidato cha kwanza katika shule hiyo na wakati mwingine mwanafunzi huyo  alikuwa  analala nyumbani kwa Mwalimu  wake huyo kwa siku kadhaa, kama mkewe.

Vyanzo  vimeeleza kuwa mwalimu huyo ambaye anafundisha somo la jiografia alifanikiwa kumtongoza na kumrubuni mwanafunzi huyo tangu akiwa kidato cha kwanza kwa kumwongezea maksi kila mtihani unapofanyika.

Baada ya wazazi wa mtoto kufuatilia nyendo za mtoto baada ya kupotea kwa siku tatu mfululizo, wazazi walitoa taarifa  Central Polisi Mbeya ambapo Polisi walianza kufuatilia.

Siku tatu baadaye, mwanafunzi huyo wa kike alirejea nyumbani kwao. Wazazi walimpeleka Polisi. Alipobanwa, aliwaambia Polisi kuwa ametoka  kwa mwalimu Mapunda na kukiri kufanya naye ngono bila kinga.

Habari za kiuchunguzi zimeeleza kuwa Polisi na wazazi waliamua kwenda kumpima afya katika hospitali ya rufaa ya Mbeya ambapo majibu yalionesha kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ameambukizwa VVU.

Uchunguzi umebaini kuwa, jalada la uchunguzi wa polisi lipo chini ya askari anayefahamika kwa jina la Andrea Mwambembe na askari mwingine aliyefahamika kwa jina la Mwashiwuya.

Lakini katika hali ya kustaajabisha, inadaiwa askari hao walipokuwa wakifuatilia sakata hilo kwa kumfuata mwalimu Mapunda kazini kwake, walipofika, Mkurungenzi wa shule hiyo aliyefahamika kwa jina la Shukran Mwasajobe alimshitua Mwl. Mapunda  na kusababisha kutorokea wilayani Chunya.

Siku iliyofuata Shukran anadaiwa kumfuata Afande Justine Kayombe na Afande mwanaume  lakini mwenye simu iliyosajiliwa kwa jina la Judith Juma, ili kumalizazana na tatizo hilo.

Katika hali ya kushangaza, Shukran baada ya kukutana na askari hao na kuweka mambo sawa, alionekana akimfokea askari  Sponsor Millinga na kwenda kumlalamikia kuwa anatafuta rushwa kwake.

Taarifa zinaonyesha kuwa hadi sasa mwalimu Mapunda hajakamatwa kwa kosa lolote na mwanafunzi aliyebakwa ameshindwa kufanya mtihani huku wazazi wakilalamika.

Kwa sasa mwalimu Mapunda, Shukran na Afande Justine Kayombe wanadaiwa kuwa maswahiba na mara kadhaa wanaonekana wakiwa pamoja katika hoteli ya Moon Dust iliyopo kata ya  Ruanda eneo la Soweto Mkoani Mbeya.

Taarifa kutoka Ofisi za Ukaguzi kanda zinaonyesha kuwa mwalimu huyo  amekuwa na kashfa ya ngono tangu akiwa katika Shule ya Montifot Sekondari iliyopo Usangu wilayani Mbarali mkoani Mbeya, na alifukuzwa hapo kabla ya mwakza 2008 baada ya kutuhumiwa kosa kama hilo, la kufanya mapenzi na mwanafunzi.

Taarifa kutoka kwenye familia ya mwalimu huyo  zinaonyesha kuwa  kati ya mwaka 2007, muda mfupi kabla hajafukuzwa kazi katika Shule ya Montifot, mwalimu huyo alianza kukorofishana na mkewe katika suala la ufuska na walipohamia jijini Mbeya, mkewe alimfumania akiwa na mwanafunzi wa kike ndani na hivyo ndoa yao kuvunjika papo hapo, huku mkewe akirejea nyumbani kwao mkoani Tanga.

Ili kuzima sakata hilo, Mkurugenzi wa shule hiyo anadaiwa kutaka kumfukuza Mkuu wa shule hiyo ambaye anaonekana kuhoji mara kadhaa juu ya sakata hilo ili hali yeye tayari anadhani amelimaliza polisi.
Previous
Next Post »