Kuanzia sasa ni marufuku kutoa pongezi, pole


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni za Bunge ambaye pia ni Naibu Spika, Job Ndugai



























KUANZIA sasa Bunge limepitisha kanuni za kuwabana mawaziri kutoa salamu za pongezi, shukrani na pole pindi wanapokuwa wakizungumza bungeni. Pia mawaziri hao wamezuiwa kutaja majina ya wabunge waliochangia bajeti zao kwa kuwa kufanya hivyo ni kutumia vibaya muda wa Bunge.

Kauli hiyo, ilitolewa bungeni jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni za Bunge ambaye pia ni Naibu Spika, Job Ndugai, alipokuwa akiwasilisha Azimio la Marekebisho ya Kanuni za Bunge.

Pamoja na mambo mengine, Naibu Spika alitoa kauli hiyo alipokuwa akifafanua kauli ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), aliyeonyesha kutoridhishwa na jinsi Spika wa Bunge anavyotumia Kanuni za Bunge juu ya matumizi ya muda.
Previous
Next Post »