HIKI NDICHO KILICHOSABABISHA BALOTELLI KUFUNGIWA


 
Matukio yamekuwa kama ndiyo rafiki wa karibu wa Mario Balotelli kutokana na mchezaji huyu wa Milan kufungiwa kucheza mechi 3 za ligi ya Serie A, na hii ni kufuatia kitendo chake cha Jumapili cha kumtukana refa aliyekuwa anachezesha mechi yao dhidi ya Fiorentina.
 
Wakati haya yanampata, Tayari mchezaji huyu alikuwa akose mechi moja kutokana na kadi za njano alizokuwa nazo, na sasa ana mechi mbili zaidi atakazozikosa kwa kumtukana muamuzi msaidizi mwishoni kabisa mwa game.
Haya ndiyo maneno ambayo yamemponza Balotelli ["What the f*** are you looking at?"]
Kwa sasa pia msakata kabumbu huyu anasubiria kulipa faini baada ya kukamatwa akivuta sigara katika choo cha treni waliyokuwa wamepanda na timu yake huko Florence.
Game ambazo Balotelli hatazicheza ni kati ya Milan na Napoli, Juventus na pia catania na kumbuka kuwa kwa mwaka huu mpaka sasa amecheza mechi 11 za klabu na timu ya taifa ambapo 
kati yake ana magoli 10.
Previous
Next Post »