HAYA NDIO MABILIONI YA SHILINGI WANAYOINGIZA VILABU VYA NJE KUPITIA MIKATABA NA MAKAMPUNI YA UTENGENEZAJI WA VIFAA VYA MICHEZO - SIMBA NA YANGA VIPI??

 

 
Manchester United na Liverpool ndio timu zenye udhamini mnono wa seti nzima ya mavazi ya kimichezo katika premier league msimu huu - Liverpool wakiingiza kiasi cha £25m na United wakipata £25.4m kutoka na kwa kampuni za Nike na Warrior - lakini bado mafahari hao wawili wa England wapo nyuma ya mafahari wa  Real Madrid na Barcelona.
Mkataba wa Real na adidas, ambao unaisha mwaka 2020, unakadiriwa kuwa na thamani ya £31m kwa mwaka wakati Barcelona wakiingiza £27m kwa mwaka kutoka kwa Nike. 


Chelsea wanashika nafasi ya nne wakiingiza £20m kutoka kwa adidas, Bayern Munich wanafuatia wakiwa mbele ya Inter Milan, Manchester City, AC Milan na Juventus. England imeingiza timu nne kwenye listi ya vilabu vyenye mikataba minono na kampuni za utengenezaji wa vifaa vya michezo, wakati Spain kama kawaida ikiingiza timu mbili - Ujerumani moja, na Italia ikiingiza timu 3.



Wakati tumeshuhudia vilabu ambavyo ni mfano kwetu hapa nchini vilabu vyetu vikubwa hakuna hata kimoja chenye mkataba na kampuni yoyote ya maana ya utengenezaji wa vifaa vya michezo. Kulwa na Doto zenye mamilioni ya mashabiki zimebaki kuwa maskini huku wakiishia kupewa vifaa vya michezo vyenye nembo ya moja ya kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo bila kuambulia chochote kupitia promotion wanayoifanyia kampuni hiyo husika. Huku kampuni hiyo ikiwa inafyatua jezi za timu hizo na kuziuza kisha kutengeneza faida kubwa huku vilabu vyetu vikiambulia patupu. 
Wapenzi wa Simba na Yanga wakinunua jezi feki za timu zao

Viongozi wa vilabu vyetu fuateni mfano bora wa timu kama Real, Barca na United na kuhakikisha timu zenu zinapata kile kinachostahili kupitia kuitangaza kampuni ya vifaa inayotengeneza karibia jezi za timu zote zinazoshiriki ligi kuu ya Tanzania.
Previous
Next Post »