Barabara rasmi kutoka mji mkuu Mogadishu, kuelekea mji muhimu
wa Kusini Magharibi mwa nchi Baidoa, umedhibitiwa na wanajeshi wa Muungano wa
Afrika kutoka kwa wapiganaji wa kiisilamu.
Ni mara ya kwanza kwa barabara inayounganisha miji hiyo kuwa wazi kwa zaidi ya miaka miwili.
Kundi hilo limelazimika kuondoka katika miji mikubwa lakini wangali wanadhibiti vijiji na maeneo mengi ya mashinani.
Sehemu ya mwisho ya barabara hiyo kutoka Mogadishu, ilidhibitiwa siku ya Jumatatu , kwa mujibu wa muungano wa Afrika ambao una majeshi 18,000 nchini humo.
Muungano huo ulisema kuwa hatua hii muhimu hairuhusu tu uhuru wa watu kutembea, lakini pia inafungua njia ya kusafirishia msaada wa kibinadamu.
Wakati huoho, mlipuko ulitokea mjini Mogadishu, katika ofisi ya Dahabshiil, moja ya kampuni kubwa za biashara ya kutuma pesa barani Afrika,
Mtu mmoja alijeruhiwa wakati wa shambulio hilo.
Haijulikani aliyehusika na shambulio hilo lakini kampuni hiyo ilitishia kufunga ofisi zake katika maeneo yanayodhibitiwa na al-Shabab.
Licha ya shambulio hilo, hali imeimarika mjini Mogadishu tangu al-Shabab kuondoka mjini humo mwezi Agosti, , lakini wapiganaji wake wangali wanafanya mashambulizi ya kuvizia.
EmoticonEmoticon