Zahanati ya kijiji cha Malangali ambayo mwanafunzi huyo
alikuwa akipima na sasa ameamua kuikwepa zahanati hiyo kukwepa mkono wa
sheria ** Kufuatia sakata hilo Diwani viti maalumu atishiwa
kuuwawa
** Polisi waingilia kati sakata hilo
Mkazi wa Kijiji cha Mpona Kata ya Totowe Wilaya ya Chunya
Mkoani Mbeya anatuhumiwa kumwachisha masomo mwanafunzi wa kidato cha pili katika
Shule ya Sekondari Totowe kwa kumuoa kisha kumpa
ujauzito.
Mwananchi huyo aliyefahamika kwa jina la Ndugu Shigala
Mwachanya anatuhumiwa kutenda kosa hilo kwa kumpa ujauzito mwanafunzi
aliyejulikana kwa jina la Ngolo Jiguma(19) ambaye amesitisha masomo yake
kutokana na ujauzito alionayo ambapo wazazi walipatana kulipana Ng’ombe 45 kama
fidia ambapo tayari Ng’ombe 20 wameshatolewa.
Aidha kutokana na Mwanafunzi huyo kutambua kuwa Wazazi
wake wametenda kosa ameamriwa kuto hudhulia kliniki katika kituo cha afya cha
Malangali na badala yake amekuwa akienda katika Zahanati ya Totowe ili kukwepa
kukutwa na vyombo vya sheria
Uongozi wa Kijiji hicho umeanza kulifuatilia sakata hilo
baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mkuu wa Shule aliyokuwa akisomaMwanafunzi
huyo Frank Mwakisyala ambapo juhudi hizo zinaonekana kugonga ukuta kutokana na
kutishiwa kuawa na mtuhumiwa.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho Ndugu Yaledi Mwanguku
amesema kuwa suala hilo lipo juu ya uwezo wake hivyo alilazimika kulipeleka
suala hilo kwenye uongozi wa kata kwa ajili ya hatua zaidi za
kisheria.
Diwani wa Viti Maalumu kata hiyo Christina Kibwana ambaye
alionekana kulipokea suala hilo na kuanza kulifuatilia pia alidai kuwa alipokea
ujumbe mfupi wa maandishi ukimtaka ahame kijijini hapo lasivyo aache
kulifuatilia sakata hilo na asipoacha angeuawa.
Diwani huyo amesema ujumbe huo wenye maneno ya kutishia
yalikutwa kwenye barua nje kidogo nje ya nyumba yake ambapo aliongeza kuwa baada
ya kuona hali hiyo aliamua kutoa taarifa katika kituo kidogo cha Polisi cha
Galula Wilayani Chunya.
Diwani huyo ameendelea kulalamika kuwa baada ya kutoa
taarifa katika kituo hicho hakuna dalili wala hatua zozote zilizochukuliwa
ambapo alisema kuna dalili za Rushwa ambayo inasemekana kuwa Polisi walipewa
Rushwa ya Shilingi Milioni Moja na Nusu(1500,000/=).
Amesema kutokana na kutoonekana kwa hatua zozote aliamua
kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Chunya ambapo walimkamata
mtuhumiwa huyo kisha kufunguliwa kesi katika Mahakama ya Wilaya ya
Chunya.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Totowe kupitia Chama
cha Mapinduzi, Godian Wangala amethibitisha kutokea kwa matukio yote hayo na
kuongeza kuwa amesikitishwa na kitendo cha Mwananchi huyo pamoja na wazazi kwa
kumwachisha masomo na kumsababishia Mwanafunzi kumnyima haki ya kupata
elimu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amekiri
kupokea taarifa hizo na kuahidi kulifanyia kazi kwa ukaribu zaidi na kuhakikisha
wahusika watachukuliwa hatua zinazostahili.
Na E . Kamanga Chunya Mbeya
|
EmoticonEmoticon