Nelson Mandela alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika
Kusini
Nelson Mandela alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika
Kusini
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amelazwa tena
hospitalini baada ya kuugua ugonjwa wa mapafu kwa mara nyingine.
Taarifa kutoka kwa serikali ya nchi hiyo, ilisema kuwa Mandela mwenye umri wa
miaka 94 alilazwa hospitalini muda mfupi kabla ya saa sita usiku.
Mandela alilazwa siku kumi na nane hospitalini mwezi Disemba mwaka jana
kupokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu na kibofu.
Anasifika sana kama baba wa taifa hilo kwa kuongoza vita dhidi ya utawala wa
ubaguzi wa rangi.
Kadhalika Mandela alihudumu kama rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini tangu
mwaka 1994 hadi mwaka 1999, ingawa hali yake ya kiafya imezua wasiwasi kwa muda
sasa.
Rais Jacob Zuma alimtumia taarifa ya kumpa pole na kumtakia kupona
Mandela
"tunawataka watu wa Afrika Kusini pamoja na duniani kote kuwa watulivu na
kumuombea Madiba na familia yake. Tuna imani kuwa kikosi cha madaktari
wanaomtibu Mandela watafanya kila hali kuhakikisha anapona,'' alisema Zuma
katika taarifa yake.
Mapema mwezi huu bwana Mandela alilazwa hospitalini mjini Pretoria baada ya
kufanyiwa ukaguzi wa kiafya.
EmoticonEmoticon