HUSSEIN MACHOZI AIBIWA GESTI! MKALI wa Bongo Fleva, Hussein Machozi amelizwa vitu
vyake mbalimbali ikiwemo kompyuta mpakato ‘laptop’ katika gesti aliyokuwa
amefikia iitwayo Stanley mjini Singida.
Chanzo chetu kilichoomba kuhifadhiwa kilisema tukio
hilo lilitokea Ijumaa Machi 8, 2013 katika gesti hiyo ambapo staa huyo alikwenda
kufanya shoo na alipomaliza alipitia kwenye kikao cha kupanga mikakati ya shoo
nyingine iliyoandaliwa na Seif Shabani ‘Matonya’.
Aliporudi sasa ndipo akakuta vitu vyake havipo na
maelezo ya wahudumu yalikuwa yanamchanganya tu ndipo akaamua kwenda polisi. Cha
kushangaza aliporudi alikamatwa na kuwekwa ndani kwa maelezo kuwa alifanya
vurugu kwenye sehemu ya biashara,” kilieleza chanzo
hicho.
Kikaongeza: “Mmiliki wa gesti hiyo aitwaye
Halingumu ndiye aliyempeleka ndani.”
Akifafanua juu ya tukio hilo, Hussein Machozi
alisema: “Ni kweli hilo tukio lilitokea. Laptop yangu yenye thamani ya milioni
mbili ilipotea hivihivi kaka. Kilichoniuma zaidi ni mimi kwenda kushitaki halafu
narudi nakamatwa na kugeuziwa kibao.
“Nililala ndani usiku mmoja, nikaachiwa Jumamosi
asubuhi (Machi 9, 2013) kwa kusingiziwa kufanya vurugu na kujeruhi, kitu ambacho
si kweli.”
EmoticonEmoticon