Matukio baada ya kutangazwa mshindi Kenya


Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto
 
Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa urais nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta ameshinda na kuepuka raundi ya pili ya uchaguzi.
Lakini tume ya uchaguzi itakagua hesabu hiyo kabla ya kutangaza matokeo baadaye leo jumamosi, siku tano baada ya wakenya kupiga kura. Uhuru amepata asilimia hamsini nukta sufuri tatu na kuzuia kutokea kwa duru ya pili ya uchaguzi.
Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila Odinga akipata 5,340,546
Hata hivyo tume ya uchaguzi itatangaza matokeo rasmi baadaye leo mwendo wa saa tano asubuhi saa za Afrika Mashariki
Popote ulipo kama mkenya au mwana Afrika Mashariki tupe maoni yako kuhusu yanayojiri pale ilipo wasiliana na si kupitia ukurasa wetu wa Bofya facebook na tutayaweka maoni hayo kwenye mtandao wetu Bofya bbcswahili.com

07:47 Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wameimba wimbo wa taifa wakiwa kando ya majengo ya bunge kusherehekea ushindi wa mgombea wao


07:39 Mjini Eldoret ngome ya William Ruto mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta sherehe zimeanza mapema na asubuhi baada ya matokeo kudhihirika wazi kuwa Uhuru Kenyatta ndiye mshindi

07:35 Hanif Mohhamed wa Mombasa-Kenya kupitia ukurasa wa Bofya facebook naona mustakabali wa Kenya ni giza tupu, saa hii anasema anatafakari njia mubadala ya kukumbana na changa moto zitakazo wapata kama wakenya baada ya athari kuanza kuchimbuka.
07:26 Vifijo na nderemeo pamoja na milio ya honi katika barabara ya Kijabe mjini Nairobi kufuatia ushindi wa Uhuru Kenyatta

07:08Alex Mulwa kupitia ukurasa wa Bofya facebook anasema kuwa wakenya wamechagua viongozi ambao wataleta maendeleo na kuleta mabadiliko katika nchi yao. Alex ,kwa niaba ya wakenya anaomba ICC isitishe na kusimamisha kesi dhidi ya Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto ili kuwapa nafasi kuongoza bila wasiwasi

06:55 Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wameanza kujitokeza katika baadhi ya sehemu za mji mkuu Nairobi kusherehekea ushindi wake

06:46 Uhuru Kenyatta ana kura 6,173,433 wakati Raila Odinga 5,340,54. Hii inampa Uhuru ushindi wa asilimia hamsini nukta tatu ambao unahitajika chini ya katiba mpya kwa mtu kushinda uchaguzi wa rais.

06:40 Tume ya uchaguzi baadaye leo itatangaza mshindi wa uchaguzi ingawa hesabu ya kura inaonyesha Uhuru Kenyatta anaongoza kinyang'anyiro.
 
Previous
Next Post »