Kamanda Diwani akiongea na waandishi wa habari
MTU
mmoja ambaye anasadikiwa kuwa ni jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na Askari wa
Jeshi la Polisi akiwa kwenye harakati za kuteka magari katika Eneo la Mlima
Nyoka Jijini Mbeya baada ya kutokea kwa majibizano ya kurushiana
risasi.
Jambazi
huyo ni miongoni mwa watu waliokuwa wakitafutwa na Jeshi la Polisi Mkoani hapa
akituhumiwa kuhusika na mauaji ya Askari Polisi mwenye namba G 68 PC Jafari
yaliyotokea Februari 6, Mwaka huu katika eneo la Matundasi Wilayani
Chunya.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
katika Mkutano alioufanya na waandishi wa Habari Ofisini kwake ambapo alisema
tukio hilo lilitokea jana majira ya Saa 10(kumi) Alfajiri usiku wa kuamkia
Machi 27, Mwaka huu.
Kamanda
Diwani alisema kabla ya tukio majambazi wapatao wanne tayari walikuwa wameweka
mawe barabarani kwa nia ya kuteka magari ili wafanye uporaji katika eneo hilo la
Mlima Nyoka ambalo limekuwa na matukio kadhaa ya watu kuporwa mali
zao.
Alisema
Jeshi la polisi baada ya kupata habari za kutegwa mawe, askari walifika kwa
wakati kwa kuwa polisi walikuwa jirani na eneo hilo na kuweka mtego kwa kuwa
majambazi hawakuwa wameonekana kwa wakati ule.
Aliongeza
kuwa baada ya muda majambazi walipoona taa za gari walijitokeza tayari
kushambulia lakini kabla ya hapo polisi walitoa amri ya kujisalimisha kinyume
chake wakaanza kupiga risasi ovyo ndipo mashambulizi ya polisi
yakafanywa.
Diwani
alisema katika mapambano hayo alijeruhiwa jambazi mmoja kwa risasi kiunoni na
ubavuni kulia na wengine watatu walifanikiwa kutoroka ambapo Marehemu
alipowahishwa hospitali kwa matibabu daktari alibaini kuwa amekwisha
fariki.
Alisema
jambazi huyo alikutwa na silaha moja SMG yenye namba AB huku namba nyingine
zikiwa zimefutwa na magazine yake ikiwa na risasi ishirini na mbili (22) pamoja
na mapanga mawili([2).
Aliongeza
kuwa baada ya Marehemu kufanyiwa upekuzi maungoni mwake jambazi huyo alikutwa
na kitambulisho cha mkazi chenye namba B.0010453 chenye jina la Emanuel Blasius
Mdendemi aliyezaliwa mwaka 1984 eneo la Matamba wilayani Makete Mkoa wa Iringa
makazi yake ni Uwemba Mkoani Njombe.
“Jambazi
huyu amebainika kuwa ni miongoni mwa majambazi waliokuwa kwenye mtandao wa
majambazi uliokamatwa hivi karibuni kuhusiana na matukio waliyofanya Mikoa
mbalimbali ikiwemo Mbeya,Njombe na Iringa.aidha amebainika kushiriki katika
tukio la mauaji ya askari polisi PC Jafari wa kituo cha Mkwajuni – Chunya tarehe
06.02.2013.” Alisema Kamanda Diwani.
Aliongeza
kuwa ufuatiliaji wa majambazi waliotoroka unaendelea kufanywa ambapo pia
anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za wahalifu hao azitoe bila kuchelewa kwa
jeshi la polisi ili zifanyiwe kazi.
Pia
amewatahadhalisha majambazi na wahalifu wa makosa yeyote kuachana na uhalifu
kwa kuwa ni biashara isiyo na faida badala yake wafanye shughuli halali kupata
maendeleo ambazo fursa zake ni nyingi.
Picha
na Mbeya yetu
|
EmoticonEmoticon