CHEKI PICHA KIBAO KUHUSU JENGO LILILOPOROMOKA NA KUANGUKA POSTA JIJINI DAR ES SALAAM, INAHOFIWA WATU WENGI WAMEPOTEZA MAISHA NA KUJERUHIWA


1Madaktari wa kujitolea wakimhudumia mmoja wa majeruhi waliookolewa kwenye kifusi baada ya jengo linalomilikiwa kwa ubia kati ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC na kampuni ya Aliraza Investiments Ltd ya jijini Dar es salaam huku mjenzi wa jengo hilo ikiwa ni kampuni ya ujenzi ya Luck Construction Ltd, mpaka sasa uokoaji unaendelea lakini ukionekana kusuasua kutokana na ufinyu wa eneo lenyewe na vifaa hafifu vya kuokolea, bado haijafahamika kwamba ni watu wangapi wamepoteza maisha katika ajali hiyo na wangapi wamejeruhiwa , magari ya kubebea wagonjwa yamekuwa yakipishana mara kwa mara wakati yakipeleka ama majeruhi ama watu waliopoteza maisha katika tukio hilo la kusikitisha, tutawaletea taarifa zaidi kadiri tutakavyozipata 2Kamanda wa Kanda maalum ya Kipolisi mkoa wa Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova kulia akizungumza jambo na Mbunge wa kuteuliwa Mh. James Mbatia ambaye ameungana na wananchi wengine katika tukio hilo. 5
Uokoaji ukiendelea katika eneo la tukio. 6 7 8 9 10
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick akiwa katika eneo la tukio kusimamia zoezi la uokoaji. 11
Ulinzi ukiwa umeimarishwa katika eneo la tukio 12 13
Kibao hiki kinaonyesha kampuni ambazo zilikuwa zikijenga jengo hilo. 14

 
Previous
Next Post »