Mwenyekiti
wa Mtaa wa Ilolo Kati Ngambi Kulaba Ngambi amesema wananchi walikuwa wakimtuhumu
yeye kuwa anamlinda mwanamke huyo ili aendelee kuishi mtaani pale ili hali wao
hawamtaki mtaani hapo.
Wananchi
wa Mtaa wa Ilolo Kata ya Manga Jijini humo kumfukuza mtaani hapo Mwanamke anaye
fahamika kwa jina la Zainabu Zuberi akituhumiwa kuhusika na
ushirikina.
Wananchi hao ambao awali walitaka kujichukulia hatua
mkononi kwa kumpiga na kumchomea moto nyumba yake mtuhumiwa huyo walidai
kuchoshwa na maovu yanayofanywa na mwanamke huyo.
Baadhi ya matendo ya kishirikina wanayomtuhumu mwanamke
huyo kuhusika nayo ni pamoja na kujigamba kuwamaliza wanakijiji hao kwa kuwaloga
ikiwa ni pamoja na kuwaloga watoto wao kitu ambacho wanasema
kimeshatokea.
Wamedai kuwa mwanamke huyo amekuwa akiwagusa wanawake
wajawazito na mimba zao huharibika ambapo pia wanafunzi wanaotoka katika mtaa
huo wakifika Shule hushindwa kuona kabisa matukio ambayo mwanamke huyo
anahusishwa.
Walisema mwanamke huyo anatuhumiwa kujihusisha na matukio
ya kishirikina tangu ahamie mtaani hapo takribani miaka mitatu ambapo walisema
wakazi hao walimwonya mapema kuhusu tabia hiyo baada ya kufuatilia historia ya
maeneo aliyowahi kuishi.
Kwa upande wake Mume wa Mtuhumiwa huyo Sulemani Rubea(49)
amekataa mke wake kutuhumiwa kwa ushirikina ambapo aliwatupia lawama wanakijiji
kwa madai kuwa wanaendekeza udini na kutopenda maendeleo na ndiyo maana
hawawataki mtaani hapo.
Rubea ameongeza kuwa mtaani hapo hawapendi mtu wa dini ya
nyingine kujenga eneo hilo jambo ambalo lilipingwa vikali na wananchi
waliohudhuria mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo la kumjadili mtuhumiwa
huyo.
Awali mume wa mtuhumiwa huyo alikiri kuhama nyumba na
mitaa zaidi ya kumi ambapo lisema maeneo mengine alikuwa amejenga lakini
sehemunyingine alikuwa amepanga tu ingawa aligoma kusema sabbu inayomfanya ahame
maeneo hayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Kati Ngambi
Kulaba Ngambi amesema wananchi walikuwa wakimtuhumu yeye kuwa anamlinda mwanamke
huyo ili aendelee kuishi mtaani pale ili hali wao hawamtaki mtaani
hapo.
Amesema baada ya kuona wanachi wamepagawa na kutaka
kujichukulia hatua mkononi ili mlazimu kuitisha mkutano wa hadhara ikiwa na
kuitaarifu jeshi la polisi ambalo lilifika mapema eneo la Mkutano na kwatuliza
wananchi wasifanye lolote ambapo Askari hao waliondoka na
mtuhumiwa
Aidha katika mkutano huo wananchi hao kwa pamoja
waliazimia kumhamisha Mwanamke huyo Mtaani hapo katika mkutano ulihudhuriwa na
wakazi zaidi ya 200 ambao walidai kuchoshwa na hali
hiyo.
Matukio kama hayo yanayoashiria vitendo vya kishirikina
ni pamoja na tukio la hivi karibuni la watu wawili kuzikwa wakiwa hai
wakituhumiwa kuhusika na vitendo hivyo viovu ndani ya jamii.
|
EmoticonEmoticon