Eneo la
tukio la ajali hiyo.
Mashuhuda
wakishuhudia ajali hiyo, gari likiwa mtaroni.
Kushoto ni
gari ya Stive yenye namba za usajiri T 779 BZL na (kulia) ni gari lililohusika
na ajali hiyo lenye namba za usajiri T 584 BQV.
Huu ndiyo
waya wa umeme uliosababisha ajali hiyo.
Askari wa
usalama barabarani, akipima ajali hiyo.
Askari
akimkunja Stive na kumpakia katika gari lao ili kuondoka naye kumpeleka kituoni
Mabatini.
Gari la
Stive likiwa limebondeka kwa mbele lilikogongana na gari
jingine.
Gari
husika na ajali likiwa limetumbukia mtaroni.
Baadhi ya
warembo walikuwa na Stive katika gari lake ambao ni miongoni mwa washiriki wa
Movie hiyo, wakiwa eneo la tukio.
Movie mpya ya Msanii wa kuigiza sauti za Viongozi Stive
Nyerere, iliyokuwa ianze kurekodiwa leo imeingia dosari baada ya msanii huyo
kupata ajali na kuswekwa lupango katika kituo cha Polisi cha Mabatini, asubuhi
hii.
Msanii
huyo amepata ajali hiyo maeneo ya karibu kabisa na kituo cha Mabatini, wakati
akiwa na msafara wa wasanii wenzake wanaoshiriki katika Movie hoyo, wakati
wakielekea kuanza kurekodi.
Wasanii hao
pamoja na Stive, walikuwa wakitokea katika Kambi yao iliyokuwa maalum kwa
maandalizi ya kuanza kurekodi ikiwa ni pamoja na kufanyia mazoezi katika kambi
hiyo iliyodumu kwa wiki kadhaa.
Ajali hiyo
ilikuwa kama hivi:- Wakati Stive akiwa na baadhi ya washiriki wa movie yake
katika gari lake na wakiwa katika mwendo kuelekea eneo la kushuti sini zao,
ghafla aliona gari aina ya funcargo ikiwa imesimama mbele yake huku katikati ya
barabara akiwapo jamaa aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo
hilo.
Baada ya
kushindwa kusimama kwa ghafla ndipo alipoigonga gari hiyo kwa nyuma na gari hiyo
kutumbukia mtaroni.
Mashuhuda
wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Fundi umeme aliyekuwa
akisimamisha magari katika eneo hilo ili kuweza kuondoa waya wa Umeme uliokatika
na kulala katikati ya barabara huku ukiwa na moto, ili kuepusha madhara
zaidi.
Baada ya
ajali hiyo, walifika askari Polisi wakiambatana na askari wa usalama barabarani,
ambapo alianza kupima ajali hiyo huku madereva wakijibizana na fundi
aliyesimamisha magari, ambapo majibizano hayo yaliingiliwa kati na mmoja kati ya
askari waliofika eneo hilo.
Katika
majibizano hayo baina ya fundi, Askari na madereva wote wawili, ndipo kulitokea
kupishana kauli baina ya Stive na Askari huyo, aliyediriki kumuita Stive mjinga,
ambapo Stive alishindwa kuvumilia na kuamua kumjibu na ndipo alipokunjwa
'Tanganyika Jeki' na kukokotwa hadi katika gari walilokuja nalo askari hao na
kumpakia na kisha kuondoka naye kuelekea katika Kituo cha
Mabatini.
EmoticonEmoticon