BAADA ya
kupata dhamana msanii wa filamu Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu
ajipanga kujiendeleza na masomo ili aweza kupambana na changamoto za
maisha.
Akizungumza
na Maisha msanii wa filamu ambaye pia amekuwa ni mtu wa karibu familia ya Lulu
Mahfudh Hussein 'Dkt. Cheni' amebainisha kuwa Lulu yupo kwenye mchakato wa
kurudi shule ili aweze kuendelea na masomo yake
Alisema
kuwa ingawa familia ina mikakati hiyo suala kubwa linalokwamisha kwa sasa ni
kipato kwani familia yake haina uwezo wa kumlipia msanii huyo na badala yake
anatakiwa Lulu kuanza kufanya kazi ili aweze kujikwamua kwa
hilo
Dkt.
Cheni aliweka wazi kuwa kutokana na kipato cha familia ya msanii huyo hivyo
anatakiwa kwa sasa aweze kufanya kazi ya filamu ili aweze kujimudu kama
ilivyokuwa mwanzo na maisha yaendele
"Hapo
awali alikuwa na uwezo wa kuihudumia familia yake kwa njia ya kazi zake alikuwa
anamsomesha mdogo wake wa mwisho pamoja na kulipa kodi ya nyumba alikuwa
akifanya mammbo mengi hivyo na swala la kusoma lijukumu lake pia"
alisema
Mbali na
hayo msanii Cheni alieleza kuwa Lulu yupo tayari kurudi shule ili aweze
kujikwamua kielimu aweze kupambana na maisha hivyo jambo la msingi ni yeye
kufikisha malengo yake aliyojipangia kwani umri wake bado ni mdogo na ananafasi
kubwa ya kubadilisha maisha yake
Akizungumzia
kwa upande wa kazi Dkt. Cheni aliweka wazi kuwa endapo Lulu akimuomba amsimamie
kazi zake atafanya hivyo kwani yote ni katika nia njema ya kumfikisha msanii
huyo katika malengo aliyojipangia
EmoticonEmoticon