Papa Benedikto wa 16 amejiuzulu rasmi leo kama kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni. Katika hotobu yake ya mwisho kwa umati wa watu zaidi ya laki moja na nusu waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro jana, Benedikto wa 16 ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani, aligusia changamoto zilizolikumba kanisa wakati akiwa kiongozi wake, na kusema kuwa kuna wakati ilionekana kwake kama mungu amesinzia.
Hata hivyo, aliongeza kuwa mara zote alifahamu kuwa Mungu ndiye nahodha wa meli ya kanisa katoliki, na kwamba kamwe asingeiacha meli hiyo izame.
Kesho Ijumaa makardinali wataanza mchakato wa kumchagua papa mpya. Benedikti wa 16 atajulikana sasa kama Papa Emeritus, na atahamia katika chumba cha kitawa mjini Vatikani mwezi Aprili.

EmoticonEmoticon