HAPA AKIWA KITUO CHA POLISI UWANJA WA NDEGE JIJINI DAR
ES SALAAM
BAADA ya
watanzania wa kada mbali mbali kutapeliwa kwa njia mbali mbali hasa kupitia
mawasiliano ya simu hatmaye mtuhumiwa mkuu wa vitendo vya utapeli nchini ambae
anamiliki majina zaidi ya matatu kwa kutapelia watu amekamatwa jijini Dar es
Salaam.
Mtuhumiwa
huyo ambae anamiliki majina zaidi ya matano amekuwa akitapeli watu wa kada mbali
mbali wakiwemo wanahabari, walimu na hata wafanyakazi wa Hoteli na watu wengine
wengi leo amekamatwa eneo la Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam baada ya mtego
kabambe uliowekwa na mmoja kati ya wanawake waliotapeliwa ambae ni mfanyakazi wa
Hoteli moja maarufu jijini Dar es Salaam (jina
limehifadhiwa)
Mfanyakazi
huyo wa Hoteli ameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com leo kuwa
yapata siku mbili zilizopita tapeli huyo ambae alijitambulisha kwa jina la Kevin
alimpigia simu na kuwa amepata taarifa kutoka kwa mwalimu wake wa chuo cha
Hoteli na utalii kama anatafuta kazi nje ya Hoteli hiyo hivyo yeye ni meneja wa
Hoteli ya Flamingo hivyo yupo tayari kumpa ajira katika Hoteli hiyo na kama
anaowezake kama watano awaeleze kuwa nafasi ipo.
Imedaiwa
kuwa Kevin kama alivyojiita katika utapeli huo baada ya dakika chache alimpigia
tena simu mwanamke huyo na kumtaka siku ya pili wakutane katika Hoteli hiyo ya
Flamingo ili awaonyeshe mazingira ya Hoteli hiyo na kujua nini cha kufanya
.
Hata
hivyo mara baada ya kufika siku iliyopangwa kama walivyoahidiwa aliwataka kila
mmoja kutoa fedha kiasi cha shilingi 30,000 kwa ajili ya kushonewa sare za
Hoteli hiyo sare ambazo zingekuwa ni mali yao kutokana na wafanyakazi wengi kuwa
na tabia ya kukimbia na sare sasa wameamua kila anayefika kuomba kazi awe na
sare yake toka nyumbani kwake.
Alisema
kuwa baada ya kutoka kiasi hicho cha fedha yeye pamoja na mwenzake mmoja tapeli
huyo aliwataka kukaa nje ya Hoteli hiyo ili afanye mawasiliano na mkurugenzi
ndipo awaite ofisini na baada ya hapo kweli aliingia ofisini ila jinsi
alivyotoka haikufahamika na wao kujikuta wanakaa hadi saa 12 za jioni bila mtu
kuonekana na kuamua kuuliza kwa wahusika na ndipo walipobaini kutapeliwa baada
ya kuambiwa hakuna ajira mpya zilizotangazwa hapo na kuwapa utaratibu wa ajira
unavyotumika kutangazwa katika Hoteli hiyo.
Kutokana
na kulizwa kiasi hicho cha pesa kitu cha 60,000 kwa wawili ndipo usiku
alipompigia simu tapeli huyo na kujifanya akiulizia majibu kwa madai kuwa jana
alipatwa na msiba hivyo aliondoka mapema zaidi .
"Kweli
baada ya kumpigia simu tapeli alionekana kuwa mkali zaidi kuwa ni mambo gani
nimefanya yeye alitoka kujua kutufuata hakukututa hivyo akataka kujua lini
nitakuwa tayari kufika ili nianze kazi...na ndipo nilipomwomba nafasi yangu
nimpe mtu mwingine mimi nilidanganya kuwa nitachelewa kurudi ....ila bila kujua
nilikuwa namtega alikubali na kusema nimpe namba za huyoa atakayechukua nafasi
yangu na wengine wawili kama wapo...na hapo ndipo nilipoweka mtego na leo
tumemkamata"
Tapeli
huyo amekuwa akijiita majina mbali mbali likiwemo la Abdalah Mkwachu, Aman kwa
namba hizi 0713094986,07162404425
Pia inadaiwa ndie aliyepata
kutapeli watu kupitia ajira hewa za TGNP kwa kutumia jina la Lilian
Dihalo, mwenye namba za simu 0717-196386 ila pia inasadikika ndie
aliyewaliza wanahabari wengi nchini kupitia jina la Zuhura
Kambangwa.
Mbali ya
makundi hayo tapeli huyo anadaiwa kuwatapeli walimu na watu mbali mbali maarufu
nchini kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi.
EmoticonEmoticon