Hoyce Temu
akimpa mkono wa pole mke wa Marehemu Daudi Mwangosi alipoitembelea familia hiyo
kuifariji.
Mwanaharakati
wa kijamii Hoyce Temu kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania amefanya ziara
mkoani Iringa na kupitia nyumbani kwa familia ya mwandishi aliyeuawa Daudi
Mwangosi na kuwajulia hali.
Hoyce Temu
kwa pamoja na kundi zima la waandaaji wa kipindi cha mimi ni Tanzania waliwasili
katika nyumba ya mjane huyo Bi. Itika Mwangosi kumsabahi na kutaka kujua
anaendeleaje na maisha kila siku.
Hoyce Temu
akimfariji mke wa Marehemu Daudi Mwangosi Bi. Itika Mwangosi alipoitembelea
familia hiyo mkoani Iringa.
Ziara hiyo
nyumbani hapo ni kwa nia nzuri ya kutaka kujua jinsi anavyokabiliana na
changamoto za kila siku za maisha pamoja na watoto wake
wanne.
Walizungumza
mengi yakiwemo yale yanayomkwaza Bi. Itika Mwangosi na jitihada anazofanya ili
kujikwamua.
Aidha Bi.
Temu akiwa amewapakata watoto wa marehemu aliifariji familia hiyo akiwataka
kutokata tamaa na kuwa Mungu yupo na kwa kuwa watanzania ni wamoja mambo
yatakwenda sawa.
Hoyce Temu
akiwapa kumbatio la upendo watoto wa marehemu Daudi
Mwangosi.
Bi. Itika
Mwangosi akionyesha uso wa matumaini baada ya kupewa maeneo ya faraja na Hoyce
Temu.
Amezungumza
na watoto kuhusu kwenda shule na kutaka kujua wanasoma shule gani na iko umbali
gani kutoka nyumbani.
Pamoja na
mambo mengine Hoyce Temu kupitia kipindi cha Mimi na Tanzania amewasihi
watanzania wenye moyo wa ukarimu kumsaidia Mjane huyo ambaye hana ajira kwa
hivyo ni vigumu kupata kipato cha kujitosheleza yeye na wanawe kwa mahitaji
muhimu ya kila siku.
Watoto wa
Marehemu wakionyesha matumaini mapya baada ya kufarijiwa na Hoyce Temu.
Mtanzania
mwenye ufariji kwa familia hiyo anaweza kutuma kiasi chochote cha fedha kwenye
namba inayomilikiwa na mjane huyo Mama Itika Mwangosi kupitia mtandao wa M-Pesa:
0767670739 ili msaada huo uwafikie walengwa.
EmoticonEmoticon