DIVA LOVENESS LOVE : NATANGAZA NIA YA KUGOMBANIA UBUNGE KIGOMA MWAKA 2015

 
“Nataka 2015 nikagombanie Ubunge Kigoma , swali kugombania ubunge Kigoma ni Lazima niwe mzawa wa Kigoma? ilov Kigoma,” ni tweet ya mtangazaji wa Clouds FM, Loveness aka Diva aliyoandika saa sita mchana Jumapili hii.
Kama watu wengi walivyomzoea, walijua ameamua kujifurahisha tu kwa kuandika kitu ambacho kamwe hakiwezi.
Lakini Diva alionesha kuwa huo sio utani na kweli amedhamiria. ‘This is not a Joke , nataka kugombania ubunge Kigoma 2015 , Diva future North Kigoma MP, anyone got a Qn, ask! Nantashinda,” alisisitiza.
“Na ntatumia njia inaitwa strength of a woman, u should put that woman first mind games tu and coz got mad lov for kigoma#mpalltheway.”
Kwanini anataka kugombea Kigoma na sio sehemu nyingine? “People wako nice, charming , wanaheshima, wanakubali cha kwao na wana support,” alifafanua.
“Coz Kigoma kuna ardhi, mbuga za wanyama, lake Tanganyika uvuvi and what more??? Vitu vingi sana ,ntasema.”
Amedai kuwa hivi sasa anajifunza Kiha na hivi karibuni ataenda mkoani humo.
“Diva Kigoma future MP, my campaign manager atakuwa@linex_tz , he is training me hicho kilugha cha Kigoma, soon ntaenda.”
Katika kile kinachoonesha watu wengi kumpuuzia kwa kauli hiyo, walimuuliza maswali ambayo mengi yalikuwa ya kejeli lakini alijibu kusisitiza nia yake na kuanza kujinadi.
‘Najua ntaimarisha vipi elimu, ajira na kilimo, nataka wajiajiri na biashara ndogondogo ,mikopo midogo midogo itawasaidia sana.”
“Kwanini nishindwe? Labda nikuulize! Nani kakwambia navaa high heels 247? Nani kakwambia siwezi zunguka vijijini?” alimtupia swali mmoja aliyeonesha mashaka naye kwa kumchukulia kama sista duu!
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe wa jimbo ambalo Diva ataliwania kwa madai kuwa yeye atakuwa ‘rais mtarajiwa’ ameonesha kumuunga mkono mtangazaji huyo kwa kusema, “Kila raia mwenye sifa za kikatiba anaweza kuwa mbunge. Bunge linareflect jamii. Acha watu wawe huru kusema watakacho. Hakuna ujinga ulio ujinga mtupu, hata ktk ujinga kuna kujifunza.

Naye Diva aliongezea, “Am free to say whatever I believe kinafaa. As long As sijamtukana mtu, nasema nautaka ubunge Kigoma by hooks and crooks. Ndo nshachagua huko sasa , no one can fight me or change me, maamuzi, nakutaka sana huko kigoma ndo uamuzi wangu. Mimi sio mzawa ni mzalendo, tunavunja imani ya uzawa ili tulete mabadiliko, ntajiunga na chama kitanipitisha,wananchi watakubali.”
Mjadala uliendelea kuwa mzito. ‘Bado nina mashaka sana kukumbusha tu wanawake wangapi waligombania majimbo wakashinda mpaka sasa ndo tuendelee,” aliambiwa na mtu mmoja nay eye kujibu, “Walishindwa wao, ungenijua ungejua nilivyokuwa na misimamo mikali na sitetereki, nina jiamini, nguzo ya mwanamke kujiamini.”
“Last but not least ! No one can fight me, by hooks and cooks, Diva for kigoma as future MP, vote vote vote , muda ukifika!”

Alimalizia kwa kusema, “It was only a teaser, sneak peak #staytunned2015.
Previous
Next Post »