Precision Air kuzindua safari za Mbeya karibuni

 
2news2jan2013
Shirika la Ndege la Precision, linatarajia kuzindua rasmi ruti mpya ya safari za kuelekea jijini Mbeya katikati ya mwezi huu, ikiwa ni takriban mwezi mmoja toka uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mbeya, uanze kutumika rasmi.
Kuzinduliwa kwa ruti ya Mbeya, kutalifanya shirika hilo kuwa na jumla ya ruti 16, na shirika hili limepanga kufanya safari hizi mara nne kwa wiki katika ruti hii ambayo ina umbali wa takriban kilomita 680, huku ikitarajiwa kuwa ndege yao mpya iliyozinduliwa hivi karibuni ya ATR 42-600, itatumika kwa safari hizi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Air, Alfonse Kioko, uzinduzi wa safari hii utakuwa na manufaa makubwa kwa uchumi wa taifa, wakazi wa Mbeya na hususan sekta ya utalii.
“Tunajivunia kuzindua njia hii mpya ya safari zetu kuelekea Mbeya, Tunaamini kuwa itatoa fursa kwa watalii zaidi kutembelea eneo hilo na tutahakikisha kuwa tunatoa huduma hizo kwa gharama ambazo ziko ndani ya uwezo wa watu wengi” amesema mkurugenzi huyo.
Previous
Next Post »