Mpango wa Sumatra kutoa leseni kwa kampuni sasa waiva


MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), inatarajia kuanza kutekeleza utaratibu mpya wa utoaji leseni za usafiri wa abiria Dar es Salaam kupitia kampuni za usafirishaji au ushirika wa watoa huduma.
Hatua hiyo inalenga wamiliki wa vyombo vya usafiri kujiandaa kushiriki katika mradi wa mabasi yaendayo kasi, kwani kutakuwa na kampuni chache zenye uwezo wa kutoa huduma bora na mabasi yenye viwango.
Akizungumza Dar es Salaam jana kuhusu mkutano wa utaratibu mpya wa utoaji leseni, Meneja Uhusiano wa Sumatra, David Mziray alisema zoezi hilo linatarajia kuanza Julai Mosi, mwaka huu.
“Tumechukua hatua ya kubadili utaratibu wa utoaji leseni kama njia mojawapo ya kuboresha mfumo wa utoaji huduma Dar es Salaam... Hii itasaidia kwa pande zote kwa wamiliki na sisi kama wadhibiti,” alisema Mziray.
Alisema wamiliki wataweza kufanya biashara ya usafirishaji kwa weledi na ufanisi zaidi na kwamba, wao kama wadhibiti watawasimamia watoa huduma wachache.
Alisema hatua hiyo itaimarisha shughuli za udhibiti na kuwa na usafiri bora na salama kwa wananchi.
Kuhusu mkutano huo, Mziray alisema utafanyika Februari 5, mwaka huu na kwamba utawajumuisha wamiliki wote wa mabasi ya daladala yanayotoa huduma Dar es Salaam.
Alisema katika mkutano huo wataalamu kutoka vyombo vya fedha, msajili wa Kampuni na Alama za Biashara (Brela) na baadhi ya wasafirishaji kutoka nchi jirani, watapata nafasi ya kubadilishana uzoefu kwa kutoa mada zinazolenga kufanikisha mfumo huo mpya.
Meneja huyo alitoa wito kwa wamiliki wote wa daladala Dar es Salaam kushiriki mkutano huo na kwamba, mawakala, madereva na makondakta hawataruhusiwa kuhudhuria.

Previous
Next Post »

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng