KESI ya mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi imeahirishwa tena katika mahakama ya hakimu Mkazi kwa kile kinachoelezwa kuwa upelelezi haujakamilika na hakimu anayeendesha kesi hiyo kutokuwepo mahakamani hapo.
Kesi hiyo ya mauaji inayomkabili askari, Pacificus Clephase mwenye namba G2372 imeahirishwa jana mbele ya Hakimu, Mary Senapel baada ya hakimu anayesimamia kesi hiyo, Daines Lyimo kutokuwapo mahakamani hapo pamoja na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.
Kesi hiyo ya mauaji inayomkabili askari, Pacificus Clephase mwenye namba G2372 imeahirishwa jana mbele ya Hakimu, Mary Senapel baada ya hakimu anayesimamia kesi hiyo, Daines Lyimo kutokuwapo mahakamani hapo pamoja na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.
Akizungumza na Mwananchi nje ya mahakama, Wakili wa Serikali, Aldof Maganda alisema kesi hiyo imeairishwa kwa kuwa upelelezi haujakamilika lakini pia ni kutokana na hakimu anayesikiliza kesi hiyo kutokuwepo mahakamani hapo.Maganda alisema, kutokuwepo kwa hakimu anayesimamia kesi hiyo haina maana kuwa mtuhumiwa hatofikishwa mahakamani bali kesi hiyo huarishwa na kupangiwa tarehe nyingine.
Kesi hiyo iliyofunguliwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya askari huyo, imekuwa ikiahirishwa mara kwa mara kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo mtuhumiwa kuugua, Serikali kukosa mafuta ya gari ya kumfikisha mtuhumiwa mahakamani na jana ya hakimu kutokufika mahakamani.
Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2, mwaka huu katika Kijiji cha Nyololo alipokuwa akiwajibika katika kazi zake za kutafuta habari wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kufanya mikutano ya ndani ya kuimarisha chama.
EmoticonEmoticon