Assad alaani wapinzani kuwa magaidi

Rais Assad akihutubia wafuasi mjini Damascus

Katika hotuba yake ya mwanzo ya taifa tangu mwezi wa Juni, Rais Bashar al-Assad wa Syria amelaani tena upinzani kuwa ni magaidi wanaosaidiwa na mataifa ya nje, na alipendekeza ile aliyoita suluhu ya siasa ya kumaliza vita
Akihutubia wafuasi waliomshangilia kwenye jumba la tamasha za opera mjini Damascus, Rais Assad alieleza pendekezo lake la kuwa na mkutano wa mapatano ya taifa ambao utaandika katiba mpya.
Lakini alisema hatazungumza na wale aliowaita karagosi wa mataifa ya Magharibi.
Kundi la upinzani la National Coalition in Syria, lilitoa maanani hotuba hiyo ya Rais Assad.
Msemaji wa NCS alinena kuwa rais anataka kuchafua makubaliano yoyote ya kimataifa ambayo yanaweza kumaliza utawala wake.
Previous
Next Post »