Watu 4 wakamatwa Afrika Kusini-ANC

Wajumbe wa ANC


Njama ya kushambila mkutano wa wajumbe wakuu wa chama tawala nchini Afrika Kusini, cha African national Congress ANC, imetibuliwa.

Msemaji wa polisi nchini humo amethibitisha tukio hilo, na kusema kuwa washukiwa wanne wenye asili ya kizungu wenya itikadi za siasa kali wamekamatwa.



Rais Jacob Zuma, na maafisa wengine wakuu wa serikali na wa chama hicho wanaohudhuria mkutano huo unaoendelea Mangaung, wamepewa ulinzi mkali.

Viongozi wapya wa chama hicho wanatarajiwa kuchaguliwa na wajumbe hao.

Chama cha ANC, kimekuwa madarakani tangu kumalizika kwa utawala wa wazungu walio wachache mwaka wa 1994.

Msemaji wa polisi Phuti Setati, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa washukiwa wanne ambao walikuwa wakipanga jinsi ya kuuweka bomu katika eneo la mkutano huo, unaofanyika katika chuo kikuu cha Free State iliyoko katika eneo la Mangaung.

Zuma kukabiliana na naibu wake


Mwandishi wa BBC Milton Nkosi, ambaye yuko katika eneo hilo anasema, hali ya ulinzi imeimarisha nje na ndani ya ukumbi wa mkutano huo.

Ameongeza kusema kuwa maafisa wa polisi wanayakagua magari yote na watu wanaoingia katika ukumbi huo kwa kutumia vifaa maalum na pia mbwa wa kunusa.

Rais Jacon Zuma
Rais Jacon Zuma na naibu wake

Rais Jacob Zuma aliufungua mkutano huo siku ya Jumapili na anawania muhula wa pili kuwa kiongozi wa chama cha ANC.

Hata hivyo Bwana Zuma, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa naibu wake Kgalema Motlanthe.

Mmoja wa wafanyabiashara tajiri zaidi nchini Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, amemuunga mkono rais Zuma kwa kuwania kiti cha naibu kiongozi wa chama hicho.

Bwana Ramaphosa alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliochangia pakubwa wakati wa mpito kutoka kwa utawala wa kizungu hadi kwa utawa wa Afrika walio wengi.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, katika eneo hilo la Mangaung, ambako chama hicho kiliundwa karibu karne moja iliyopita, rais Zum,a alisema kuwa Afrika Kusini iko tayari kwa awamu ya pili, ambayo atahakikisha kuafikiwa na maendeleo ya kijamii na kiuchumu yatayaokuwa na manufaa kwa raia wa nchi hiyo.

Matokeo ya uchaguzi wa viongozi wakuu wa chama hicho yanatarajiwa baadaye wiki hii.
Previous
Next Post »