KIDOTI


Tulipokuwa tunaelekea mwishoni mwa wiki iliyopita,kuna jambo jipya lilikuwa linatokea. Jokate Mwegelo ambaye kwa wengi hahitaji utambulisho wa kina,alikuwa akizindua kampuni yake inayokwenda kwa jina la Kidoti Loving ambayo itajikita zaidi katika bidhaa mbalimbali zinazoendana na masuala ya urembo.Kwa kuanzia, Jokate alizitambulisha aina nane za nywele(weaving) ambazo Kidoti Loving tayari nimeshaziingiza sokoni.

 Mtu ambaye naweza kusema ndio alichangia kwa mapana zaidi jina la “Kidoti” ni mdogo wake rafiki yangu wa karibu sana. Ilikuwa mwaka jana na nakumbuka nilikuwa kwenye pressure ya kutafuta jina la kuweka kwenye meza kwenye hafla ya Red Ribbon. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kushiriki na mwandaaji mkuu wa Red Ribbon Gala,Khadijah Mwanamboka alikuwa akihitaji jina la designs zangu. Nikiwa kwenye pressure hiyo yule mdogo wake rafiki yangu ndio akaniambia kwanini usiziite Kidoti? Basi nikajikuta nasema tu zinaitwa Kidoti na kuanzia hapo ndio jina la Kidoti likawa rasmi na ndio mpaka sasa limeshazoeleka hivyo.



Previous
Next Post »