Bomu lauwa waumini wane Kaduna, Nigeria

Mji wa Kaduna, NIgeria
Kumetokea mripuko mkubwa wa bomu kwenye kanisa la Kikatoliki katika mji wa Kaduna, kaskazini mwa Nigeria
Mwandishi wa BBC huko anaarifu kuwa shambulio hilo lilitokana na bomu lilotegwa kwenye gari liloripuliwa na mtu aliyejitolea mhanga, na kugonga gari hilo kwenye ukuta wa kanisa.
Anasema uharibifu mkubwa umetokea ndani ya jengo na kwamba mapaa ya maduka na nyumba za karibu yaling'oka.
Afisa wa kanisa alisema watu kama wane waliuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Wakuu wanasema vijana wa Kikristo walioingiwa na hasira kwa sababu ya tukio hilo, walishambulia gari la serikali ambalo lilikwenda kusaidia manusura.
Kumetokea mashambulio kadha ya kidini katika jimbo hilo, mengi yamefanywa na kundi la wapiganaji wa kiislamu, Boko Haram.
Previous
Next Post »