Watu zaidi ya 30 wameuwawa Tana River-Kenya.

Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya limesema mapigano baina ya makabila mawili ya ndani yanayojishughulisha na mifugo na kilimo kusinimashariki mwa nchi hiyo yamepamba moto Jumatatu huku watu 38 wakiwa wameuwawa wakiwemo polisi tisa.

Katibu mkuu wa shirika la Msalaba mwekundu Kenya Abbas Gullet amesema jumatatu kwamba watoto nane ni miongoni mwa waliouwawa katika shambulizi hilo ambalo takriban watu 300 wa kabila la pokomo walivamia kijiji cha Orma wa kabila la wafugaji. Wavamizi hao walichoma nyumba 167.

Gullet anasema ingawa makabila hayo mawili yamekuwa yakipigana mara kwa mara kugombea ardhi na vyanzo vya maji lakini ghasia za mwaka huu zinaweza kuwa na uchochezi wa kisiasa.

Ijumaa wajumbe 11 kutoka kabila la Pokomo waliuwawa na jumuiya ya Orma katika tukio la kujibu mashambulizi. Watu wa kabila la Pokomo mapema waliwauwa wajumbe 52 wa Orma.
Previous
Next Post »