UNAWEZA KUDHIBITI U.T.I MWENYEWE..!
U.T.I ni ugonjwa sugu unaosumbua
sana watu wengi hivi sasa, wakubwa kwa wadogo. U.T.I (Urinary tract
Infection) ni ugonjwa unaoathiri njia ya mkojo na huweza kusababisha
maumivu makali na unapojiimarisha mwilini kwa muda mrefu huathiri figo
pia. Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na mtu kusikia haja ya kukojoa kila
wakati na kusisimka wakati wa kujisaidia, kusikia maumivu, kutoa mkojo
mchafu na hata kutoa haja ndogo iliyochanganyika na damu.
Wataalamu wetu wa masuala ya tiba wanatueleza kuwa tatizo hili
hujitokeza pale mlango wa njia ya haja ndogo inaposhambuliwa na bakteria
ambao husambaa na wasipotibiwa mapema huenea hadi kwenye figo na athari
zake ni mbaya.
UNAWEZA KUDHIBITI U.T.I KWA TIBA MBADALA
Kwa kawaida kila ungonjwa una tiba mbadala, siyo lazima kwenda
hospitali. Unaweza kuudhibiti au kuponya ugonjwa huu kwa kunywa maji
mengi pamoja na juisi itokanayo na matunda halisi, iwapo utawahi kabla
tatizo halijawa sugu.
Kwa maana nyingine, unaweza kujikinga na ugonjwa huu kwa kuwa na mazoea
ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Ukinywa maji ya kutosha yatakufanya
uende haja ndogo kila mara na kwa njia hiyo wale bakteria watakuwa
wakitoka na hatimaye kuisha kabisa. Aidha, njia nyingine ya kuudhibitibi
ugonjwa huu ni kunywa maji mengi au kwenda haja ndogo mara baada ya
kufanya tendo la ndoa, kitendo hiki husaidia kuwaondoa mapema bakteria
wote ulioambukizwa wakati wa kujamiiana na mwenzio.
Katika hali ya kawaida, ugonjwa wa UTI hutoweka ndani ya siku tatu mara
baada ya kuanza kutumia tiba asili ya kunywa maji mengi na juisi ya
matunda halisi, iwapo ugonjwa utaendelea kuwepo baada ya siku hizo, hiyo
itakuwa na maana ugonjwa wako umeshakomaa na hivyo hauwezi kutibika kwa
tiba hii ya nyumbani.
Katika hali kama hii, utakuwa huna njia nyingine isipokuwa kwenda
hospitalini na kuonana na daktari ambaye atakufanyia uchunguzi na
kukupatia dozi sahihi ambayo utatakiwa kuizingatia bila kukosa. Uamuzi
huu ni muhimu hasa kama unasikia maumivu makali ambayo yanaweza kuwa
yanasababishwa na kuathirika kwa figo. Kwa kawaida tiba ya kidaktari kwa
ugonjwa huu huhusisha matumizi ya dawa kali za ‘antibiotics’, ambazo
watu wengi wanazikimbia kutokana na athari zake za baadae (side
effects). Lakini ni muhimu kufuata ushauri wa dokta na kumaliza dozi ili
kuepuka uwezekano wa kurejea kwa ugonjwa, tena kwa kasi kubwa.
KUZUIA
Ili kujiepusha na ugonjwa huu, suala la usafi na kuwa na tabia ya kunywa
maji ya kutosha ni jambo muhimu sana. Hakikisha unajisafisha vizuri
mara baada ya kwenda haja na kubadilisha mara kwa mara nguo yako ya
ndani, hasa kwa akina mama.
Vile vile usikae na haja ndogo kwa muda mrefu, nenda kajisaidie mara
nyingi kadri unavyosikia kufanya hivyo. Kitu cha mwisho cha kuzingatia
kwa mgonjwa wa UTI ni kupunguza unywaji wa pombe na vinywaji vingine
vyenye sukari, kwa sababu sukari ni chakula cha bakteria hivyo kwa
kuendelea kunywa kinywaji chenye sukari kutaifanya hali kuendelea kuwa
mbaya. Ugonjwa huu ni rahisi kuepuka kwa mtu anayependa kunywa maji ya
kutosha na kunywa juisi halisi kila siku.
DAYATI MUHIMU KUDHIBITI UTI
Katika kuudhibiti ugonjwa huu, pendelea kula vyakula ama vinywaji vyenye
kiwango kikubwa cha vitamini C ambayo utakipata kwenye matunda ya aina
mbalimbali yakiwemo machungwa, mboga za majani n.k. Jiepushe na ulaji wa
vyakula vya ‘kupaki’ kama vile ‘chizi’, chokoleti na bidhaa nyingine
zilizotengenezwa kutokana na maziwa. Pia jiepushe na ulaji wa vyakula
vyenye viungo vingi kama pilau, epuka vyinywaji vyenye ‘caffeine’,
kilevi na sigara na mwisho achana na vinywaji kama soda na vinavyofanana
na soda.
EmoticonEmoticon