PATCHO MWAMBA: SIJAONANA NA MMILIKI WA FM ACADEMIA ZAIDI YA MIAKA MIWILI

PATCHO MWAMBA: SIJAONANA NA MMILIKI WA FM ACADEMIA ZAIDI YA MIAKA MIWILI

MWANAMUZIKI supa staa wa FM Academia, Patcho Mwamba amesema kwa zaidi ya miaka miwili hajaonana na mmiliki wa bendi hiyo.
Hata hivyo Patcho Mwamba ambaye pia anatesa katika filamu, aliiambia Saluti5 kuwa hajutii jambo hilo kwa vile haoni ulazima wa kufanya hivyo hasa kwa vile bendi yao ina safu nzuri ya utawala, kitu kinachopelekea kukosekana ulazima wa yeye kuonana na tajiri yake.
“Kuna safu iliyojipanga vizuri kuanzia kiongozi wa wanamuziki hadi meneja wa bendi, mshahara unapatikana, makubaliano yangu na bendi yanatekelezwa sasa kwanini nimtafute tajiri? alihoji Patcho.
“Kitendo cha tajiri kufikiwa kirahisi na wanamuziki ndio mwanzo wa majungu, mimi sina shida ya kuonana na tajiri, bado sijapata sababu ya msingi ya kumtafuta, nina zaidi ya miaka miwili sijamuona na pengine tukikutana naweza kuwa nimemsahau” alisema Patcho na kufichua kuwa tajiri yake huyo si mtu wa kutokea kwenye maonyesho ya FM Academia.
FM Academia iliyoanzishwa miaka 15 iliyopita na kupitia kwa wamiliki tofauti tofauti, kwasasa inamilikiwa na Martin Kasyanju.
Previous
Next Post »