
RAIS wa kwanza wa FM Academia, Lous Katorz amesema kipato cha wanamuziki wa dansi hapa nchini kiko chini kiasi kwamba hata mtu ajibane vipi hawezi kununua japo baiskeli kwa mshahara wake.
Amesema wanamuziki wanaonufaika ni wachache huku wanaoumia ni wengi.
Akiongea katika ofisi za Saluti5 Katorz alisema kuwa wengi kati ya wale wanaoonekana kuneemeka, hawajanufaika kwa mishahara yao bali ni kwa mambo mengine.
“Faida pekee katika muziki wa dansi ni kupata umaarufu, wako wanaoutumia umaarufu wao kama ngazi ya kutengeneza vyanzo vingine vya pesa na ni hao wanaonufaika japo pia si wote.
“Lakini wenye nyuso za aibu wakashindwa kuutumia umaarufu wao kama ngazi, ni maumivu kwao.
“Nimeamua kupumzika muziki wa jukwani, nahisi haunisaidii kitu, najipanga ili niweze kufungua studio hapo baade” alisema Katorz.
Katorz ndiye kiongozi wa kwanza wa FM Academia pale ilipoanzishwa miaka 15 iliyopia, ni mkali wa kucharaza drum na gitaa la bass, ni bingwa wa kupangilia muziki na ni mtunzi mkali. Moja ya nyimbo kali alizozitungia FM Academia ni “Hadija” uliochuana sana na wimbo “Neema” wa wapinzani wao wa jadi enzi hizo, Diamond Sound “Wana ikibinda nkoi”
EmoticonEmoticon