TAMBUA DALILI YA BAADHI YA MAGONJWA KWA KUTAZAMA ULIMI WAKO.

Bila shaka umewahi kwenda hospitali kuonana na daktari na ukajikuta ukiambiwa utoe ulimi nje ili daktari aangalie ulimi wako.Wengine wetu tunafahamu kuwa ulimi matumizi yake ni kutusaidia katika kutambua ladha, kusaidia katika kuunda maneno wakati wa kuzungumza.

Hata hivyo, madaktari wanaeleza kuwa unaweza kufahamu maradhi anayougua mtu kwa kuangalia ulimi wake tu, kutokana na kiungo hicho kuwa na uwezo wa kuonesha dalili za iwapo mtu ana homa, kikohozi, kisonono,kichwa, tumbo,kisonono na maradhi yanayohusiana na HIV pamoja na kufeli kwa ogani za mwili.

Ulimi wenye afya kwa kawaida unatakiwa uwe msafi, wenye rangi ya pinki na wenye vitonetone ambavyo ndivyo hutumika kubainisha ladha mbalimbali.

Hata hivyo kwa kawaida ulimi wenye rangi nyekundu au mweupe ni dalili ya kuwa na maradhi kama fangasi.Kadhalika ulimi uliovimba ni dalili kubwa ya mtu kuwa na mzio.Pia ulimi ni mojawapo ya kipimo kinachoweza kuonesha iwapo kinga ya mwili imeshuka.

Yote hayo ni kutokana na kiungo hiki kuwa na uhusiano mkubwa na mwili wa binadamu na ogani za ndani ya mwili.Kwa mfano, anasema ulimi kuwa na weupe mithili ya maziwa ya mgando ni dalili ya fangasi na maradhi ya kinywa mengine yanayohusiana na zinaa.

Wataalamu wa afya wanasema ulimi wenye rangi nyeusi au usio na rangi ni dalili kubwa kuwa mtu huyo ametumia kwa muda mrefu dawa za antibayotiki au ongezeko la fangasi kwa mtu anayeishi na Virusi vya Ukimwi.

Ili kutumia ulimi kama kipimo,vitu vifuatavyo huangaliwa ikiwa ni pamoja na rangi yake, umbile, yaliyomo kwenye ulimi, unyevu wake, ukubwa na ulaini wake.Pamoja na hayo,ulimi ni kigezo tosha cha kujua iwapo mtu anaugua magonjwa ya zinaa, kama ulimi una mistari mirefu hiyo ni dalili ya magonjwa ya zinaa. 
Previous
Next Post »