"Simtambui Dkt. Shein kama Rais wa Zanzibar
Nataka tu kuweka rekodi sawa. Nilimpinga Dkt. Ali Mohamed Shein
hadharani na jana bungeni. Alipoingia Shein bungeni sikusimama kama
inavyotakiwa. Nilikaa chini kupinga uhalali wake.
Alipoingia Rais John Magufuli nilisimama na kumpa heshima yake kama Rais
na kukaa kumsikiliza. Kuendelea kuzomea wakati Rais halali kaingia
Bungeni kuzindua Bunge ili wabunge waanze kazi ni kutokuwa na mikakati
sahihi. Ilitosha kumzomea Shein na kukaa chini bila kusimama alipoingia
kama tulivyofanya. Wenzangu hawakujua pa kuishia.
Magufuli anapambana na rushwa. Mimi napambana na rushwa. Namwunga mkono katika vita dhidi ya rushwa.
Anayempinga Magufuli kwa vyovyote vile anatetea wala rushwa na mafisadi.
Anayempinga Magufuli ni yule anayeogopa viwanda na mashamba
yaliyobinafsishwa kurudishwa Kwa umma".
-Zitto Z Kabwe
EmoticonEmoticon