Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli akihutubia wananchi katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro .
Watu
wawili wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na mkanyagano
uliotokea jana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika mkutano wa kampeni za
mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli.
Tayari
leo, Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Jakaya Kikwete amewatembelea majeruhi hao waliolazwa
Hospitali ya Mkoa Morogoro.
Mganga
Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Ritha Lyamuya amesema walipokea watu 19
waliokuwa na majeraha yakiwemo ya kuvunjika maeneo mbalimbali ya mwili
na kuongeza kuwa miongoni mwao, wawili walikufa kutokana na kuumia
vibaya.
Aidha Dk Lyamuya alisema kuwa wagonjwa ambao bado wamelazwa wako 10 na wengine saba walitibiwa na kuruhusiwa.
Dk
Lyamuya alisema kuwa waliokufa ni pamoja na mwanamke anayekadiriwa kuwa
na umri wa miaka 42 na mtoto wa umri wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina
la Ramadhan Abdalah.
Uwanja
wa Jamhuri jana ulifurika watu wakati mgombea urais kwa tiketi ya CCM
John Magufuli alipokwenda kwa ajili ya kufanya kampeni.
Mara
tu baada ya Magufuli na viongozi wengine kuondoka uwanjani hapo, ndipo
hali ya kusukumana na kukanyagana ilitokea getini wakati watu wakitoka.
EmoticonEmoticon