Mwenyekiti
wa maandalizi ya Tamasha la Kuombea Amani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25,
Alex Msama akifafanua jambo kuhusu maandalizi ya tamasha hilo jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni mwimbaji wa nyimbo za injili, Christopher Mwahangila na
Upendo Nkone. (Picha na Francis Dande)
Mwimbaji wa nyimbo za injili, John Lissu akiimba kwa hisia moja ya nyimbo zake wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya Tamasha la kuombea Amani Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, tamasha hilo limeandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions na litakafanyika Oktoba 4 kwenye Uwanja wa Taifa. Kushoto ni mwimbaji Christopher Mwahangila na Upendo Nkone.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, John Lissu akiimba kwa hisia moja ya nyimbo zake wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya Tamasha la kuombea Amani Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, tamasha hilo limeandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions na litakafanyika Oktoba 4 kwenye Uwanja wa Taifa. Kushoto ni mwimbaji Christopher Mwahangila na Upendo Nkone.
Mwimbaji
wa nyimbo za injili, Jesca Honore 'BM' akiimba wimbo wa 'Napokea' Jesca
ni mmoja wa waimbaji watakaopamba tamasha la Amani la kuombea Uchaguzi
Mkuu na Taifa.
WAIMBAJI mahiri wa nyimbo za injili nchini waliotajwa
kushiriki Tamasha la Uchaguzi Mkuu litakalofanyika Oktoba 4, katika Uwanja wa
Taifa, jijini Dar es Salaam, wameelezea walivyojipanga
kufanikisha malengo ya tukio hilo
la kihistoria.
Wakizungumzia
Tamasha hilo kwa nyakati tofauti katika
mkutano wa utambulisho wao, baadhi ya waimbaji waliothibitishwa, wameelezea
kufurahia kuwa miongoni mwa waimbaji watakaotumbuiza maelfu katika tamasha hilo la kuombea amani na
utulivu Uchaguzi Mkuu.
Kwa
upande wake Upendo Nkone, alisema ni faraja kwake kuwa miongoni mwao waimbaji
katika tukio hilo
la kumsihi Mungu ajalie hali ya amani na utulivu wakati na baada ya uchaguzi
mkuu kwani amani ndio msingi wa mafanikio ya kila kitu.
“Nafarijika
kuwemo katika orodha ya waimbaji katika Tamasha hilo. Watanzania tukumbuke taifa linahitaji
maombi kwani linapita katika kipindi kigumu ambacho bila msaada wa Mungu, ni
mtihani mgumu ambao katika nchi nyingi tu, umekuwa chanzo cha mifarakano,”
alisema Upendo.
Naye
Christopher Mwangila, mbali ya kushukuru kupata nafasi hiyo, pia amewasihi
wapendwa katika Kristio Yesu, wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili
kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya kupaza sauti kwa Mungu autangulie uchaguzi
huo uwe wa amani.
Kauli
hiyo iliungwa mkono na mwimbaji mwingine, John Lissu ambaye pamoja na shukrani
kupata nafasi ya kushiriki, pia ametumia fursa hiyo kuwasihi wapenzi na
mashabiki wa muziki wa njili na wote wenye upendo kwa
nchi yao
kujitokeza siku hiyo.
Naye
Matha Mwaipaja, alisema anamshukuru Mungu kupata fursa na kumjalia kipaji cha
uimbaji, hivyo ana kila sababu kushiriki tukio muhimu kama hilo la kuombea amani ya nchi kwa kuzingatia
kuwa, viongozi hutoka kwa Mungu.
Mwimbaji
mwingine aliyetoa neno kuelekea Tamasha hilo,
ni Jesca Boniface Magupa ‘BM’ akisema amejiandaa vizuri kuipamba siku hiyo
akishirikiana na wengine mahiri wa ndani na nje ya nchi akiamini sauti za
kumsihi Mungu uchaguzi uwe wa amani, hazitapotea bure.
EmoticonEmoticon