Meneja
wa kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Mwanza, Raymond
Richmond,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampuni hiyo kutumia
mapumba ya mchele na mashudu ya pamba,kama chanzo cha nishati ya umeme
kinachotumika kuendeshea mitambo.Kushoto ni Meneja wa Maji na Nishati wa
kampuni hiyo, Sunday Kidolezi.
Meneja
wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond,
akizungumzia mradi wa matumizi ya mapumba ya mchele na mashudu ya
pamba,ambacho ni chanzo cha nishati ya kuendesha mitambo kiwandani
hapo.Nishati ni rafiki wa mazingira kwa sababu haina hewa ukaa.Wanaokoa
Dola za Kimarekani (USD) 400,000 hadi 500,000 kwa mwaka ambazo
zingetumika kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendeshea mitambo .
Waandishi
wa habari wakiongozwa na Meneja wa Kiwanda cha kampuni ya Bia (TBL)
Mwanza, Raymond Richmond(wa kwanza kushoto), kwenda kutembelea mtambo
unaotumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba kuzalisha nishati ya
umeme inyotumika kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa
Maji na Nishati wa TBL, Sunday Kidolezi.
Meneja
wa Nishati na Maji wa Kampuni ya Bia (TBL)Mwanza, Sunday Kidolezi (wa
kwanza kulia),wakiwa na waandishi wa habari wakati wakitembelea mtambo
wa kuzalisha umeme kwa kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba.wa
Kwanza kutoka kushoto (mwenye shati jeupe), Ni Meneja wa Kiwanda hicho,
Raymond Richmond.
Meneja
wa Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,Raymond Richmond (mwenye shati jeupe)
akiwaonesha waandishi wa habari mtambo unaozalisha nishati ya umeme kwa
kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba kwa ajili ya kuendesha
mitambo ya kiwanda hicho.anaoshuhudia ni Meneja wa Maji na Nishati wa
kampuni hiyo,Sunday Kidolezi (mwenye fulana ya mistari).Mwingine ni
mwandishi wa habari wa kampuni ya The Guardian, Daniel Mkate,ambaye ni
miongoni mwa waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho.
Raymond
Richmond, Meneja wa kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,akiwaonesha waandishi
wa habari (hawapo pichani), mapumba ya mchele,yanayotumika kuzalisha
nishati ya umeme wa kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja
wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo.
Mwandishi
wa habari, Daniel Mkate (kushoto) akiwauliza maswali, Meneja wa
Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond na Meneja wa Maji na
Nishati wa kampuni hiyo, Sunday Kidolezi, kuhusu changamoto ya
upatikanaji wa mali ghafi hiyo na madhara yake katika kuzalisha nishati
na athari za mazingira.
Wafanyakazi
wa kiwanda cha Kampuni ya Bi (TBL) Mwanza,wakijaza mapumba kwenye
magunia, kabla ya kuingizwa kwenye mtambo wa kuzalisha umeme kiwandani
hapo.Hapo ni katika eneo linalotumika kupakulia shehena ya mapumba hayo
ya mchele, kutoka kwa msambazaji.
Meneja
wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,Raymond Richmod,
akiwaonyesha waandishi wa habari, Daniel Mkate wa TRhe Guardian (nyuma)
na Henry Kavirondo wa Chanel Ten,mashine inayosukuma mapumba ya mchele
na mashudu ya pamba, kwenda kwenye mtambo wa kufua umeme unaotumika
kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa
kampuni hiyo, Sunday Kidolezi.
Wafanyakazi
wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,wakijaza mapumba ya mchele
kwenye mashine kwa ajili ya kuyasukuma kadi kwenye mtambo wa kuzalisha
nishati ya umeme, unaotumiwa kuendesha mitambo ya uzalishaji ya kiwanda
hicho.
Meneja
wa Maji na Nishati wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Sunday
Kidolezi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhudu mradi huo wa
uzalishaji wa nishati ya umeme,unaotumika kuendesha mitambo ya kiwanda
cha kampuni hiyo kwa kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba.Wa
kwanza kushoto ni Meneja wa kiwanda cha kampuni hiyo,Raymond Richmond.
KONA YA JAMII
NEWS
UMEME WA PUMBA ZA MCHELE, MASHUDU YA PAMBA WATUMIKA KUENDESHEA MITAMBO YA TBL MWANZA
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon