MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA BASI MALI YA KAMPUNI YA SAI BABA KUGONGA LORI LILILOKUWA LIMEEGESHWA.



       TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
   PRESS RELEASE” TAREHE 22.09.2015.


·         WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA BAADA YA BAJAJI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUGONGA GARI.


·         MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA BAJAJI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.


·         MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA BASI MALI YA KAMPUNI YA SAI BABA KUGONGA LORI LILILOKUWA LIMEEGESHWA.


KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ABILAH PHILIMON (17) MKAZI WA ILEMI, DEREVA WA BAJAJI NA 2. BARAKA SELEMANI (23) MKAZI WA SIMIKE WALIFARIKI DUNIA BAADA YA BAJAJI YENYE NAMBA ZA USAJILI MC 276 APL ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA MAREHEMU KUGONGA GARI  T.588 AMR AINA YA MITSUBISHI FUSO ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA EMANUEL FRANSIS (35).
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 21.09.2015 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO KIJIJI CHA HATWELO, KATA YA HATWELO, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO, WATU SITA KATI YAO WANAUME WATANO NA MWANAMKE MMOJA WALIJERUHIWA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA BAJAJI. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA, MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALINI HAPO.


KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA MKAZI WA TEWELE – NAKONDE –ZAMBIA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRAID AINKALA (67) AFARIKI DUNIA BAADA YA BAJAJI YENYE NAMBA ZA USAJILI MC 630 AFC IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 21.09.2015 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KIJIJI CHA NKANGAMO, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, BARABARA KUU YA TUNDUMA/SUMBAWANGA.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO, WATU WAWILI WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. MAGRETH MTAMBO (52) NA 2. ANASTAZIA NYAMUNGALA (55) WOTE WAKAZI WA KAKOZI –NAKONDE – ZAMBIA.  CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA NA MAJERUHI WAMELAZWA KITUONI HAPO.




KATIKA TUKIO LA TATU:
MTU MMOJA AMBAYE BADO KUFAHAMIKA JINA LAKE, TINGO WA BASI MALI YA KAMPUNI YA SAI BABA AFARIKI DUNIA BAADA YA BASI HILO LENYE NAMBA ZA USAJILI T.668 BLD AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKITOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA SUMBAWANGA KUGONGA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.771 ATV/T.771 AUU SCANIA LORI ILIYOKUWA IMEEGESHWA BAADA YA KUHARIBIKA ENEO LA MLIMA NYOKA.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 21.09.2015 MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU HUKO ENEO LA MLIMA NYOKA, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/NJOMBE.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO, ABIRIA WAWILI AMBAO PIA MAJINA YAO BADO KUFAHAMIKA WALIJERUHIWA NA WOTE WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA BASI HILO. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA/MICHORO NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA WA BASI LA SAIBABA AZITOE ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »