Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo,
kushoto, akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya
simu za mikononi aina ya Huawei ijulikanayo kama 'Jibayportphonishe',
uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Micka Mavoa,
Mkurugenzi wa Cape View, Kampuni inayoshirikiana na Bayport katika
huduma hiyo ambayo mteja akikopa simu atapelekewa hadi mahala
anapohitaji ifike. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIKA
hali isiyokuwa ya kawaida, Taasisi ya kifedha ya Bayport Financial
Services, imezindua huduma yake mpya ya kukopesha (Smartphone) simu za
mikononi aina ya Huawei zenye thamani ya Sh 140,000, ikiwa na lengo la
kuwawezesha Watanzania ambao ni watumishi wa umma na wafanyakazi wa
kampuni binafsi zilizoidhinishwa kumiliki simu wakati wowote ili
ziwakwamuwe katika suala zima la mawasiliano ya simu za mikononi, huduma
inayotambulika kama 'Jibayportphonishe'.
Kuanzishwa
kwa huduma hiyo ya mikopo ya simu za mikononi kumekuja siku chache
baada ya taasisi hiyo pia kuzindua huduma ya bima ya magari, pikipiki na
bajaj, ambapo zote kwa pamoja ni mkombozi kwa Watanzania, wakiwamo wale
wenye kipato cha chini na cha kati.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja Masoko na Mawasiliano wa
Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba kuanzishwa kwa
huduma hiyo kutaifanya jamii iwe katika kiwango kizuri cha mawasiliano,
hivyo kukuza pia uchumi wao.
Mkurugenzi wa Cape View, Micka Mavoa, kulia akizungumza jambo.
Alisema
kwamba badala ya mtumishi wa umma na wale wa kampuni binafsi
zilizoidhinishwa kuwekeza kidogo kidogo ili wanunuwe simu watakazo, sasa
wanaweza kukopeshwa simu hizo na kupelekewa hadi katika maeneo yao
wanayopatikana. Alisema simu hizo zitaambatana na ofa ya intaneti MB 500
bure kila mwezi kwa miezi sita kutoka katika Kampuni ya Simu za
Mikononi ya Vodacom Tanzania, huku mteja akilazimika kulipa Sh 9000 kila
mwezi, katika kipindi cha miezi 24.
“Bayport
Financial Services ni taasisi ya Watanzania wote wakiwamo wale wenye
kipato kikubwa au kidogo, hivyo kwa kuanzishwa kwa huduma hii, mteja
wetu anaweza kukopa simu kisha akalipa kidogp kidogo, ukizingatia kwamba
wapo watoto wanaosoma mbali na wazazi wao, hivyo naamini kwa fursa hii
hata maisha yatakuwa rahisi.
“Baba
au mama anaweza kuchukua simu apendazo kwa ajili ya familia yake, ambapo
pia akichukua simu yenye malipo kwa kipindi cha miezi 60, atalazimika
kukatwa Sh 6000 tu kila mwezi, ikiwa ni huduma rahisi na nzuri kwao,
hivyo Bayport tunaamini wateja wetu na Watanzania kwa ujumla wataendelea
kutuunga mkono ili tuwahudumie na kuwakwamua zaidi,” alisema.
Naye
Mkurugenzi wa Cape View, Micka Mavoa, alisema kwamba huduma hiyo mpya ni
muhimu kwa Watanzania wote bila kuangalia kipato chao, ukizingatia
kwamba wanaweza kufikishiwa simu hadi majumbani kwao baada ya mkopo wao
kufanikiwa.“Kwa kushirikiana na Bayport Financial Services, tunaamini
kwa kiasi kikubwa tutafanikiwa kwenye huduma hii, ukizingatia simu hizi
ni nzuri na zitakuwa na waranti ya mwaka mmoja ili kuona wateja wetu na
Watanzania kwa ujumla wanapata huduma bora, huku simu hizo zikiwaa na
huduma zote za mitandao kama vile WhatsApp, Facebook, Twitter, na
mengineyo bila kusahau ofa ya vifurushi vya internet kutoka Vodacom bure
kwa kipindi cha miezi sita,” alisema.
Kwa
mujibu wa Ngula, ili mtu aweze kukopeshwa simu hizo kwa watumishi wa
umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi zilizoidhinishwa na Bayport,
anatakiwa kutembelea tawi la ofisi ya Bayport zilizoenea nchi nzima au
kwa wakala na kupewa fomu ya mkopo na endapo utaidhinishwa atafanikiwa
kupata simu hizo kwa kufikishiwa hadi eneo analoishi ndani ya siku tatu
tu.
Bayport
ni taasisi ya kifedha inayotoa huduma bora za kifedha, ambapo imekuwa
ikizindua huduma mbalimbali kama vile mikopo ya bidhaa, viwanja vya
mradi wa Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, mikopo ya fedha na
nyinginezo zinazowakwamua kiuchumi wateja wao ambao ni watumishi wa umma
na wafanyakazi wa kampuni binafsi zilizoidhinishwa na Bayport, huku
huduma hizo zikitolewa pia kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz.
EmoticonEmoticon