Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akisaini
hati ya makubaliano ya mkopo nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Benki
ya Dunia ili kuimarisha sekta ya afya nchini katika hafla iliyofanyika
jana jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini
Tanzania Bi Bella Bird.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto)
akibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo nafuu na Mkurugenzi wa Benki
ya Dunia nchini Tanzania Bi Bella Bird (kulia) mara baada ya kusaini
hati hiyo ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia
ili kuimarisha sekta ya afya nchini jana jijini Dar es salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akiongea na
waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kuimarisha
sekta ya afya nchini jana jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa
Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi Bella Bird.
Mkurugenzi
wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi Bella Bird (kulia) akiongea na
waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kuimarisha
sekta ya afya nchini jana jijini Dar es salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Dkt. Deo Mtasiwa (kulia) akisisitiza jambo wakati hafla ya
usatiji saini hati ya makubaliano kuimarisha sekta ya afya nchini kati
ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia jana jijini Dar es salaam.
Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambaye pia ni Mkurugenzi
wa Mipango na Sera Bernard Konga (kulia) akitoa shukrani kwa Serikali ya
Tanzania na Benki ya Dunia kwa kuthamini sekta ya afya jijini Dar es
salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Deo Mtasiwa.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto)
akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi
Bella Bird baada ya kuasini hati ya makubaliano ya mkopo nafuu kati ya
Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia katika kuimarisha sekta ya afya
nchini jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya waandishi wa habari na viongozi wa serikali na wawakilishi wa Benki
ya Dunia waliohudhuria hafla ya kusaini hati ya makubaliano ya mkopo
nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia katika kuimarisha
sekta ya afya nchini jana jijini Dar es salaam.(Picha Eleuteri
Mangi-MAELEZO).
Na Allen Mhina –MAELEZO
Serikali
kupitia mpango wa kuimarisha afya duniani, imepokea Dola za Kimarekani
milioni 200 sawa na Sh. Bilioni 422.8 toka Benki ya Dunia ili kuimarisha
sekta ya afya nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius
Likwelile wakati wa hafla ya kusaini hati ya makubaliano ya mpango wa
kuimarisha sekta ya afya nchini iliofanyika leo jijini Dar es salaam
kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia.
Akiongea
na waandishi wa habari na baadhi ya viongozi wa serikali na wawakilishi
wa Benki ya Dunia, Dkt. Likwelile alisema kuwa dhumuni la makubaliano
ya mpango huo ni kuwezesha na kuimarisha sekta ya afya na vitendea kazi
vitakavyowezesha uzazi salama kwa wakina mama wakati wakujifungua na
kupunguza idadi ya vifo vya watoto kutokana na mapungufu wa afya bora.
Dkt.
Liwalile, aliongeza kuwa kuna umuhimu na makusudio ya dhati kuimarisha
sekta hiyo kutokana na uwepo wa vifo vinavyozuilika kwa wakina mama na
watoto, kama inavyodhihirisha takwimu zilizotolewa wizara ya afya
kuonesha kuwa kuna kuna idadi kubwa ya watoto wanaofariki wakati wa
uzazi kwa kukosekana kwa vitendea kazi na huduma bora wakati wa
kujifungua.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi Bella Bird
ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuonesha juhudi za dhati kutekeleza
mpango huo.
Bi
Bella amesema kuwa amefurahishwa na juhudi za Serikali ya Tanzania
katika kusimamia sekta ya afya ambapo alitembelea baadhi ya vituo
wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani na kujionea hali ilivyo na kuhaidi
kushirikiana vizuri na serikali ili kukamilisha mpango huo na kuleta
mabadiliko katika sekta ya afya nchini.
Naye
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bernard Konga
aliishukuru Serikali na Benki ya Dunia kwa kuthamini sekta ya afya na
kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika kuendeleza sekta ya afya kama
ilivyokusudiwa na ili kuboresha sekta ya afya ya kuleta matokeo chanya
katika maendeleo ya taifa kwa ujumla.
EmoticonEmoticon