HAYA NDIYO MAGONJWA ZAIDI YA MATANO AMBAYO HUWEZA KUDHIBITIWA NA TUNDA LA NANASI

Kama utakuwa upo karibu sana na mitandao ya kijamii ya Mandai Herbalist Clinic basi naamini utakuwa unakumbuka kuwa Jumapili ya juzi ya Agosti 23, 2015 Tabibu Abdallah Mandai alionekana Star Tv kupitia kipindi cha Mandai afya.com akizungumzia kuhusu nanasi.

Kufuatia kipindi hicho kumekuwa na maswali mengi wengi wakihitaji kujua umuhimu na faida za tunda hilo la nanasi.

Hivyo bila hiyana nimeona ni vyema nikupe hii orodha ya faida za nanasi kwa ujumla wake kama ifuatavyo:

Mizizi ya nanasi inapochemshwa huwa ni dawa ya matatizo ya figo na kuua minyoo mwilini.

Juisi ya majani yake ni dawa ya kutibu vidonda na matatizo ya magonjwa ya ngozi na majipu.

Maua ya nanasi yanapochanganywa na asali huwa ni tiba ya mafua na kikohozi, tumia kijiko kimoja kwa siku.

Nanasi pia huwa ni msaada kwa wale wenye shida ya matatizo ya akili na kupoteza kumbukumbu.

Tunda hili pia husaidia kutibu matatizo ya tumbo, ini, magonjwa ya bandama, homa, pumu pamoja na kusaidia kuongeza maziwa kwa kinama.
MAGUFULI AMJULIA HALI NA KUMPA POLE MEYA WA JIJI LA MBEYA MH ATHANAS KAPINGA BAADA YA KUPATA AJALI Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli akimjulia hali na kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za maandalizi ya Kampeni hivi karibuni,Mh Kapunga amelazwa kwenye chumba maalum cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa mjini humo. Mmoja wa Wauguzi walioko kwenye chumba maalum cha wagonjwa mahututi (ICU),akimpa maelezo mafupi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli alipokwenda kumjulia hali n kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za maandalizi ya Kampeni hivi karibuni. Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Wauguzi walioko katika chumba maalum cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa Mbeya,mara baada ya kumjulia hali na kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za maandalizi ya Kampeni hivi karibuni. Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Meya Mama Kapinga mara baada ya kutoka kumjulia hali na kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za maandalizi ya Kampeni hivi karibuni. PICHA NA MICHUZI JR-MBEYA

Copy the BEST Traders and Make Money (One Click) : http://ow.ly/KNICZ
Previous
Next Post »

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng