Ajali za pikipiki zaendelea kusababisha vifo na majeruhi hapa nchini.


Uvunjaji wa sheria za usalama barabarani kwa madereva wa bodaboda hasa katika maeneo mbalimbali ya makutano ya barabara zimeendelea kushamiri hapa nchini na kusababisha matukio ya ajali kuongezeka ikiwemo vifo na ulemavu wa kudumu, ambapo kuanzia mwezi January hadi Mei mwaka huu, matukio ya ajali za bodaboda ni 1062 huku majeruhi wakiwa ni 992 na waliopoteza maisha ni watu 372.
Mbali na  kushuhudia baadhi ya waendesha bodaboda kuvunja sheria kwa maksudi katika makutano ya barabara ya Mandela na Buguruni, katika eneo la Tazara hali ya uvunjaji wa sheria ilionekana kuendelea bila madereva hao kujali maisha yao.
 
Katika eneo la Ubungo, baadhi ya madereva wakiwa wamebeba watu mtindo wa mshikaki na kukatisha katikati ya makutano ya barabara ya mandela, Sam Nujoma na Morogoro bila kuhofia maisha yao huku mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kipolisi kinondoni akieleza takwim ya matukio ya ajali kwa mkoa wake wa kipolisi kwa mwaka huu.
 
Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani nchini kamanda Mohamed Mpinga, mwaka jana 2014 matukio ya ajali za pikipiki nchini zilikuwa 4,169, ambapo majeruhi walikuwa 3,884 na vifo ni watu 928 ambapo kwa mwaka huu 2015 kuanzia January hadi Mei ajali ni 1062, majeruhi ni 992 na vifo ni watu.
Previous
Next Post »