Vifaa vitakavyo tumika katika zoezi la uandikishwaji wa daftrai la kudumu la wapiga kura |
Afisa mwandikishaji Msaidizi jimbo Ndugu Vicent Msolla akizungumza katika mafunzo hayo. |
Wito
umetolewa kwa waandikishaji wa daftali
la kudumu la mpiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa Biometric Voter
Registration (BVR), kupuuza kauli za baadhi ya
watu ambao wanaweza kujitokeza na
kutumia kauli za vitisho vya kisisa au vya kigaidi katika zoezi la uandikishaji
wa wapiga kura .
Kauli hiyo
imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munasa, wakati akifunga
mafunzo ya siku mbili kwa waandikishaji wa daftari hilo la kudumu
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari ya Mbeya Day
iliyopo Jijini hapa.
Mkuu huyo
wa wilaya amesema nivema wataalamu hao wakatambua kuwa baadhi ya watu wanaweza kutoa vitisho
mbalimbali kwa watu ili wasijiandikishe hivyo ni vema wakawa makini katika
kutoa elimu kwa walengwa waweze kujiandikisha.
Aidha,
kiongozi huyo aliwasihi wataalamu hao kutojiingiza kwenye matatizo ya kuboresha
au kuongeza vitu ambavyo havihusiki kwenye mfumo huo ambao serikali umeufanyia
utafiti wa kutosha na kujihakikishia ya kwamba mfumo huo umekidhi viwango vya
ubora.
Alisema,
Taifa linapenda kuona nchi inakuwa na mshikamano, tunaingia kwenye
uchaguzi tukiwa salama na tunatoka tukiwa salama na yote haya
yatafanikiwa endapo waandikishaji hao watatumika vizuri.
Aidha,
aliwataka kuzingatia ukusanya taarifa mbalimbali za uhalifu na kuzifikisha
kwenye mamlaka husika za dola hususani wageni wanaoingia nchini kinyume
cha sheria.
Hata
hivyo, Munasa aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha
kwani wataisaidia nchi kupata viongozi sahihi kwa ngazi ya Uraisi, Ubunge na
Udiwani.
Mwisho
EmoticonEmoticon