JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWSHIKILIA WATU
WAWILI WAKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI KATIKA MISAKO
MIWILI ILIYOFANYIKA MAENEO YA UYOLE JIJINI MBEYA.
KATIKA MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA MKAZI WA UYOLE KATI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA KANAN IBRAHIM (21) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI
AINA YA BOSS PAKETI 50.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 05.03.2015 MAJIRA YA SAA
14:00 MCHANA HUKO ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA
MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
AIDHA KATIKA
MSAKO WA PILI, MWANAMKE MMOJA MKAZI
WA UYOLE KATI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GRACE
MWAZELA (40) MFANYABIASHARA
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUKAMATWA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA
SERIKALI [VIROBA] AINA YA BOSS PAKETI 15
NA RIDDER PAKETI 10.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 05.03.2015 MAJIRA YA SAA
14:00 MCHANA HUKO ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA
MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI/MTUMIAJI WA POMBE HIZO. TARATIBU ZA
KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI
KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO NA NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA
JAMII KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UINGIZAJI, USAMBAZAJI NA
UUZAJI WA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
EmoticonEmoticon