TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 06.11.2014.
Ø
JESHI LA POLISI LINAWASHILIA WATU WAWILI KWA KUKAMATWA
NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO].
Ø MTU MMOJA AMEKAMATWA BAADA YA KUWAUZIA WATU
NYAMA YA MBWA.
TAARIFA YA MISAKO.
JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA
WATU WAWILI KWA KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA
WATU WAWILI 1. HASSAN ADAMU [84],
MKAZI WA ILEMI NA 2. ALPHONCE MWAKABANA
[45] MKAZI WA MWENJELWA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA
10.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 05.11.2014
MAJIRA YA SAA 14:30HRS HUKO ENEO LA ISANGA,KATA YA ISANGA,TARAFA YA
SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU YA
MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NANI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
MTU MMOJA AMEKAMATWA BAADA YA
KUWAUZIA WATU NYAMA YA MBWA.
JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA AHADI JESIKAKA [20] MKAZI WA KIJIJI CHA
NGYEKYE KWA KOSA LA KUWAUZIA WATU NYAMA
YA MBWA.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 04.11.2014
MAJIRA YA SAA 13:45HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NGYEKYE,KATA YA MATEMA,TARAFA
YA NTEMBELA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. WATU WALIOUZIWA NA KUTUMIA KITOWEO
HICHO NI 1. ENOCK NSEMWA [52] MKAZI
WA NGYEKYE 2. GEORGE NSEMWA
[26],MKAZI WA NGYEKYE NA 3. ANYANDWILE
MBWILO [29] MKAZI WA NGYEKYE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA
MAKINI HUSUSANI WANAPONUNUA VYAKULA ILI KUJIEPUSHA NA MADHARA YA KIAFYA.
Imesainiwa na:
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon