HASHIM LUNDENGA ALIZUNGUMZIA SAKATA LA UMRI WA MISS TANZANIA 2014


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjaVVkotcQM6D0_ZeM7SpHUk5TvU1kzMkjar8__fWV4e0fXr0X78iBvnfQU7C0zBK0VOKn7yQfPBFZ3BQWFE-933x27usPWlUEDFcNb5UtVzVvzXxcd5NLdLkhtu5vOctG3_8ZxLlTruyjX/s1600/DSC_0966.JPGMkurugenzi wa Rino International Agency ambao ni Waratibu wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga akiongea na waandishi wa habari juu ya sakata la umri halali wa Mrembo aliyetwaa taji hilo Mwaka huu, Sitti Mtemvu (kushoto).

 HABARI‬ MISS TZ 2014 SITTI MTEMVU, NI MISS HALALI MWENYE VIGEZO VYOTE!
Kamati ya Miss Tanzania imesema kuwa haiwezi kumvua taji Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu kwa kuwa ni Miss halali na mwenye vigezo vyote vilivyotakiwa, na amewataka watu kutoropoka kwa kuwa hawajui vigezo vinavyotakiwa
Akifafanua kuhusu suala la umri, mratibu wa mashindano hayo Hashim Lundenga amesema kuwa cheti halali walichonacho wao ni kile kinachoonesha Sitti Mtemvu kazaliwa 31 mei 1991 na si vinginevyo.
Kuhusu suala la passport na leseni zilizosambaa kwenye mitandao ya jamii zikionesha amezaliwa mwaka 1989, Lundenga amesema wao huwa hawangaali vitu hivyo wanachojali ni cheti cha kuzaliwa.
Hashimu Lundenga amesema hakuna suala la yeye kupewa rushwa, ila Sitti Mtemvu ameshinda kihalali kwa kupitishwa na Majaji.
Kuhusu tuhuma za unene amesema wao huwa hawaangalii wembamba wala ufupi, muhimu ni awe na vigezo vinavyotakiwa
Previous
Next Post »