TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 25.08.2014.
·
MTU MMOJA MKAZI WA NTOKELA WILAYA YA RUNGWE
AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI.
·
MTEMBEA KWA MIGUU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA
KUGONGWA NA GARI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIWA
WATU WATATU WAKIWA NA RISASI 23 ZA BUNDUKI AINA YA G3.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA AKIWA NYARA ZA SERIKALI.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SISALA CHAULA (75) MKAZI WA NTOKELA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA
NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.464 BCR
AINA YA TOYOTA COASTER LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE EMANUEL ANYETIKE (55) MKAZI WA MAKUNGURU.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 24.08.2014 MAJIRA YA SAA
20:00 USIKU HUKO NTOKELA, KATA YA ISONGOLE, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA
RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUKUYU. CHANZO CHA AJALI NI
MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA
RUNGWE. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO
KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUWA MAKINI HASA KWA KUZINGATIA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI PAMOJA NA MATUMIZI YAKE.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
MTEMBEA KWA MIGUU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA IPYANA MWASAJOHN (32) MKAZI WA MBANDE AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA
GARI ISIYOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI AINA YA TOYOTA CANTER LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 25.08.2014 MAJIRA YA SAA
19:15 JIONI HUKO LWANGWA, KATA YA LWANGWA, TARAFA YA BUSOKELO, WILAYA YA
RUNGWE, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA RUNGWE. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI
MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE,
VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
TAARIFA
ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU
WATATU 1. ISSA NASSORO (37) MKAZI
WA MIKOROSHINI 2. TAMAL BRUCE (24) MKAZI WA NDANDALO PAMOJA NA 3. RODRICK MTIMI (24)
MKAZI WA KYELA KATI WAKIWA NA RISASI 23
ZA BUNDUKI AINA YA G3.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 24.08.2014 MAJIRA YA SAA
20:00 USIKU KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO MAENEO YA KYELA KATI, KATA YA
KYELA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA HAO
WALIKAMATWA WAKIWA KATIKA HARAKATI/MPANGO WA KUTAKA KUZIUZA RISASI HIZO.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA
MAENEO YAO ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
KATIKA
MSAKO WA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIIKA KWA JINA LA MWAJUMA
PAUSON (32) MKAZI WA MAMBA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [05].
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 24.08.2014 MAJIRA YA SAA
16:30 JIONI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAMBA,
KIJIJI NA KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA ANAUZA POMBE HIYO NYUMBANI KWAKE. TARATIBU ZA
KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA.
KATIKA
MSAKO WA TATU:
MTU MMOJA MKAZI WA NKUNG’UNGU WILAYA YA CHUNYA AITWAYE
ATUNGANILE ANGUMBWIK (30) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA AKIWA NA NYARA YA SERIKALI NYAMA YA KONGONI KIASI CHA KILO SITA [06].
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 24.08.2014 MAJIRA YA SAA
05:00 ALFAJIRI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA RUKALYA,
KIJIJI CHA NKUNG’UNGU, KATA YA LUPA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA,
MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA NA NYARA HIYO BAADA YA KUFANYIWA UPEKUZI
KATIKA NYUMBA YAKE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI NYARA ZA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA BADALA YAKE WAFUATE TARATIBU ZA KISHERIA IKIWA NI PAMOJA NA KUPATA
KIBALI TOKA MAMLAKA HUSIKA CHA UWINDAJI.
Imesainiwa na;
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon