WACHEZAJI SABA COSTA RICA KUFANYIWA VIPIMO VYA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU.

article-2664711-1EFF5A0400000578-628_634x418Gwiji Diego Maradona amewashambulia FIFA baada ya kuagiza wachezaji saba wa Costa Rica wafanyiwe vipimo vya kutumia dawa za kuongeza nguvu zilizokatazwa kufuatia kuifunga Italia.
Gwiji huyo wa soka Argentina amesema bodi hiyo ya kandanda duniani inaonyesha kutoheshimu sheria kwa agizo.
Wachezaji wawili tu wa Italia walifanyiwa vipimo baada ya kipigo cha 1-0 kutoka kwa Costa Rica Ijumaa– na kuzima matumaini ya England kusonga mbele kutoka kwenye makundi.
Maradona, mwenye umri wa miaka 53, amesema: “Kama kuna wachezaji saba wa Costa Rican, kwa nini haiku hivyo kwa Italia?
“Hii ni mpya. Lakini hii inatokea kwa sababu imewaumiza mno watu kuona Costa Rica inasonga mbele na hao mabingwa wa dunia hawajafuzu, kwa sababu wadhamini hawatatoa fedha walizoahidi.
“Ni kinyume cha sheria. Kila inatakiwa kupeleka wachezaji wawili kwa vipimo vya dawa za kuongeza nguvu. Ilitokea kwangu, iliniumiza, hivyo nipo tayari kuzungumzia mpango huu. Lakini wachezaji saba, haiwezekani.
“Kuchukua wachezaji saba wa Costa Ricans kwa vipimo vya dawa inaomyesha kutoheshimu wachezaji na sheria. Costa Rica imefuzu kishujaa, jape ilikuwa ina mabingwa watatu wa dunia kwenye kundi na imewafunga kwa soka nzuri,
Maradona alishinda Kombe la Dunia na Argentina mwaka 1986 lakini alirudishwa nyumbani katika fainali za mwaka 1994 baada ya kugundulika alitmia dawa aina ya ephedrine wakati wa vipimo. Pia aligundulika anatumia deawa za kulebya aina ya cocaine mwaka 1991 na akafungiwa kwa miezi 15.
Ametoa maoni yake kupitia kipindi cha Televisheni ya Argentina, De Zurda.  Gazeti la Costa Rica liliwataja wachezaji saba waliofanyiwa vipimo hivyo kuwa ni Bryan Ruiz, Michael Barrantes, Keylor Navas, Celso Borges, Christian Bolanos, Marco Urena na Diego Calvo.
Gazeti hilo, El Dia limesema vipimo hivyo vinaonyesha kwamba FIFA ina wasiwasi na Costa Rica baada ya kuzifunga Uruguay na Italia.
Previous
Next Post »