·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA MKAZI WA NKUYU – KYELA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU 26 KWA KOSA LA KUNYWA POMBE KABLA YA MUDA.
MSAKO WA KWANZA:
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRANK MWAMPAJA
(40) MKAZI WA NKUYU ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA
POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 26.06.2014
MAJIRA YA SAA 11:46 ASUBUHI KATIKA
ENEO LA ITUNGI-PORT, KATA YA BULOMA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA
AKIWA NA DOUBLE PUNCH KATONI 2 NA BOSS KATONI 1. TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII NA WAFANYABIASHARA KWA UJUMLA
KUACHA KUJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU
NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA WATU/MTANDAO WA WATU
WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU ILI
WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
MSAKO WA PILI:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 26
KWA KOSA LA KUNYWA POMBE KABLA YA MUDA.
WATUHUMIWA HAO
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 26.06.2014
MAJIRA YA SAA 09:30 ASUBUHI KATIKA
MTAA WA TUKUYU – TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA
MBEYA KATIKA MSAKO MKALI ULIOFANYIKA KATIKA MAENEO HAYO.
WATUHUMIWA WOTE
WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI CC 26/2014.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUFUATA NA KUZINGATIA SHERIA ILI KUJIEPUSHA
NA MATATIZO.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
EmoticonEmoticon