TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 12.06.2014.
·
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI
KUTOKANA NA UNYANG’ANYI WA PIKIPIKI.
·
MWANAMKE MMOJA AUAWA KWA KUCHOMA KISU KICHWANI
NA MUME WAKE AKIWA AMELALA.
·
WATU WAWILI WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE WANNE
KUJERUHIWA BAADA YA MAGARI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUGONGANA NA KUPINDUKA.
·
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 03 AFARIKI DUNIA
BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
MWANAUME MMOJA ASIYEFAHAMIKA
JINA WALA MAKAZI MWENYE UMRI KATI
YA MIAKA 30-35 ALIUAWA KWA KUPIGWA
SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO, MAWE NA RUNGU KUTOKANA NA TUKIO
LA UNYANG’ANYI WA PIKIPIKI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 11.06.2014 MAJIRA YA SAA
17:30 JIONI KATIKA KIJIJI CHA IDIGA, KATA YA USONGWE, TARAFA YA BONDE LA
USONGWE, WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIMKODI
MWENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.773
CDJ AINA YA T-BETTER ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA IMANI EMANUEL (19) MKAZI WA KIJIJI CHA SONGWE NA WALIPOFIKA MBELE
ZAIDI NDIPO ALIJITOKEZA MTU MWINGINE NA KWA PAMOJA WALINYANG’ANYA PIKIPIKI NA
KISHA KUMFUNGA MIKONO NA MIGUU KWA MIPIRA NA KUTOWEKA NA PIKIPIKI HIYO.
MWENDESHA PIKIPIKI HUYO ALIFANIKIWA KUJIFUNGUA NA
KUKIMBIA KUOMBA MSAADA KWA WAENDESHA PIKIPIKI WENZAKE NA WANANCHI WA ENEO HILO
NA KUANZA KUWAFUATILIA WATUHUMIWA HAO KISHA KULIZINGILA ENEO HILO NA KUFANIKIWA
KUWAKUTA WATUHUMIWA WAKIIKOKOTA PIKIPIKI HIYO MARA BAADA YA KUISHIWA MAFUTA.
MTUHUMIWA MMOJA KATI YA WAWILI ALIKAMATWA NA KUPIGWA SEHEMU ZA KICHWANI HALI
ILIYOSABABISHA KIFO CHAKE, AIDHA MTUHUMIWA MWINGINE ALIFANIKIWA KUKIMBIA NA
KUINGIA KATIKA DIBWI LA MAJI NA KUTOKOMEA HUMO. JUHUDI ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA
TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
MWANAMKE MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA MADAWA JASTON (29) MKAZI WA KIJIJI CHA
ISANGATI ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU KICHWANI, USONI NA MIGUUNI NA MUME WAKE
AITWAYE JOSEPH JOHN (49) MKAZI WA
KIJIJI CHA ISANGATI.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NDANI YA NYUMBA ALIMOKUWA
AMELALA MAREHEMU MNAMO TAREHE 11.06.2014
MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI. TUKIO
HILO LIMETOKEA KATIKA KIJIJI CHA ISANGATI, KATA YA IHANGO, TARAFA YA TEMBELA,
WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA.
MTUHUMIWA KABLA YA KUTEKELEZA TUKIO HILO ALIMVAMIA NA
KISHA KUMCHOMA KISU MKE WAKE AKIWA AMELALA NDANI KISHA KUKIMBIA. CHANZO CHA
TUKIO BADO KINACHUNGUZWA, JUHUDI ZA KUMTAFUTA MTUHUMIWA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE
DHIDI YAKE.
KATIKA
TUKIO LA TATU:
WATU WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. RASHID MFINANGA NA 2. GODENI KATEMU (60) MKAZI WA UYOLE
WAMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA MAGARI MAWILI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA
KUGONGANA NA KISHA KUPINDUKA.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 11.06.2014 MAJIRA YA SAA
19:30 JIONI KATIKA ENEO LA KIJIJI CHA ITEWE, KATA YA INYALA, TARAFA YA TEMBELA,
WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE.
KATIKA AJALI HIYO, GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.254 BFZ AINA YA MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA RASHID MFINANGA (37) MKAZI WA MOSHI LIKITOKEA UYOLE KUELEKEA NJOMBE LILIGONGA
UBAVUNI GARI T.837 ATC AINA YA TOYOTA HAICE LILILOKUWA LIKITOKEA CHIMALA
KUELEKEA MBEYA MJINI LIKIENDESHWA NA
DEREVA MRADI CHANDE (34) MKAZI WA
KIJIJI CHA ILONGO KISHA MAGARI YOTE KUPINDUKA.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WANNE WALIJERUHIWA AMBAO
MAJINA YAO BADO KUFAHAMIKA KATI YAO WANAUME WATATU NA MWANAMKE MMOJA. CHANZO
CHA AJALI KINACHUNGUZWA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA
TUKIO LA NNE:
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 03 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA JOSHUA
SHUKRANI MKAZI WA ILEMI ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPELEKWA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA KWA MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA GARI LISILOFAHAMIKA WALA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 11.06.2014 MAJIRA YA SAA
12:15 MCHANA KATIKA ENEO LA MTAA WA MWAFUTE, KATA YA ILEMI, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA
TRANSFORMER JIJINI MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO, JITIHADA ZA
KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI
PAMOJA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
Imetolewa
na:
[AHMED Z.
MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon