MKAZI WA KIJIJI CHA LUSUNGO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA TUHUMA ZA KUIBA MTOTO MWENYE UMRI WA SIKU TANO.





TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 28.06.2014.

·         MWENDESHA PIKIPIKI MMOJA AUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI.


·         MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA LUSUNGO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA TUHUMA ZA KUIBA MTOTO MWENYE UMRI WA SIKU TANO.

·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA ZA KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA LILANGI MLAWE @ MTAFYA (38) MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA, MKAZI WA KIJIJI CHA INSANI ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUPIGWA KITU KIZITO KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KISHA KUONDOKA NA PIKIPIKI YAKE AMBAYO BADO HAIJAFAHAMIKA NAMBA ZA USAJILI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.06.2014 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU KATIKA KITONGOJI CHA NAMKOMI, KIJIJI CHA BARA, KATA NA TARAFA YA ITAKA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKODISHWA NA ABIRIA ILI AMPELEKE WILAYA YA CHUNYA KISHA KUUAWA WAKATI WAKIWA NJIANI. JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
 
KATIKA TUKIO LA PILI:

MWANAUME MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA OBEDI MAKUPA (37) MKAZI WA KIJIJI CHA LUSUNGO WILAYANI KYELA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA TUHUMA ZA KUIBA MTOTO MCHANGA MWENYE UMRI WA SIKU TANO AITWAYE DAVID SEMENI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.06.2014 MAJIRA YA SAA 04:00 ALFAJIRI KATIKA KIJIJI CHA LUSUNGO, KATA YA LUSUNGO, TARAFA YA NTEMBELA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA MTUHUMIWA KABLA YA KUTENDA KOSA HILO ALIWAVIZIA WAZAZI WA MTOTO HUYO AMBAO NI SEMENI OGADA (28) NA TUMPALE SAKWISYA (20) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA LUSUNGO WAKIWA WAMELALA USINGIZI NA KUFUNGUA MLANGO WA NYUMBA ULIOTENGENEZWA KWA MATETE KISHA KUMUIBA MTOTO NA KUKIMBIA NAE.

HATA HIVYO BABA WA MTOTO ALISHTUKA NA KUPIGA KELELE ZA KUOMBA MSAADA HIVYO MAJIRANI WALIJITOKEZA NA KUMKIMBIZA MTUHUMIWA NA KUMKAMATA AKIWA NA MTOTO HUYO. MTUHUMIWA AMEJERUHIWA BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.

MTUHUMIWA ALIOKOLEWA NA ASKARI POLISI WALIOFIKA ENEO LA TUKIO NA AMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA AKIWA CHINI YA ULINZI. AIDHA MTOTO AMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA WAZAZI AKIWA SALAMA.




MISAKO:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ADAM KYANDO (27) MFANYABIASHARA, MKAZI WA KAWETELE – CHINI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUKAMATWA AKIWA NA KETE 09 ZA DAWA ZINAZODHANIWA KUWA ZA KULEVYA AINA YA COCAINE ZENYE UZITO WA GRAM 10.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.06.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA KATIKA  NYUMBA YA  KULALA WAGENI IITWAYO UNDER  GROUND ILIYOPO MTAA WA  WAIGO,  KATA YA  KAWETELE, TARAFA YA  TUKUYU,  WILAYA YA  RUNGWE,  MKOA WA MBEYA.

KATIKA MSAKO WA PILI:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JOEL MWAKANYANGWA (24) MKAZI WA NDANDALO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO MOJA AKIWA AMEIFICHA KWENYE MFUKO WA RAMBO.   

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.06.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI KATIKA ENEO LA MACHINJIONI, KATA YA KYELA –KATI, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.

TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA KUFANYIKA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KABISA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.


                                                             Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »