Kuna taarifa kuwa watu ishirini wameuawa katika shambulio kwenye kijiji Mashariki Kaskazini mwa Kenya.
Mwandishi wa BBC anasema watu wenye silaha walivamia kijiji cha Gunana katika County ya Wajir mapema siku ya jumapili.
Amesema mapigano yalizuka kutoka na mgogoro baina ya koo mbili za Degodia na Gare.
Ni mzozo wa mpaka baina ya koo hizo ambao wakuu wanautambua, lakini bado hawakuweza kuupatia ufumbuzi.
Aidha mwandishi wa BBC ameongeza kuwa pamoja na kwamba kuliwahi kutokea mapigano mengine hapo awali lakini hayajawahi kusababisha vifo vya watu wengi kwa mara moja kama ilivyotokea siku ya jumapili.
Mauaji haya yanakuja wiki moja baada ya watu wapatao 60 kuuwawa katika mashambulizi mawili yaliyotokea eneo la Mpeketoni katika pwani ya Kenya lililodaiwa kufanywa na wapiganaji wa Al Shabaab .
Wapiganaji hao walivamia vijiji viwili karibu na mji wa Mpeketoni, na kufanya mashambulizi ambapo katika la kwanza lilisababisha mauaji ya wau 48 na baadae la pili liliua watu wapatao 20.
Chanzo BBC Swahili
EmoticonEmoticon